Monday, 16 October 2017

AFYA:VITAMBUE VIRUSI VIENEZWAVYO KWA BUSU LA MDOMONI

Image result for BLACK PEOPLE KISSING




Utafiti uliochapishwa na jarida la Microbiome la Uingereza limeonyesha kuwa upigaji busu unaweza kusafirisha zaidi ya bakteria milioni80 kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Daktari Sophianis Nyomyani wa Hospitali ya Mwananyamala anazungumzia utafiti huo na kusema  bakteria wengi ambao huambukizwa kwa njia ya busu na wengi huchukulia busu kama njia pekee ya kuonyesha upendo.

Utafiti huo pia umesema wapenzi ambao hupigana mabusu kwa wastani wa mara tisa kwa siku huwa na bakteria ambao wanaendana na hubadilishana kila wanapofanya tendo hilo.

“Ni upendo ila kiafya si salama,hata kama wanandoa wanashiriki katika kupigana busu,isiwe kwa kila mtu,ni lazima kuwe na mipaka,unaweza kumbusu mtu shavuni,nje ya mdomo,mkononi na kwingineko lakini siyo lazima mdomoni.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA