SAIKOLOJIA YA WANAWAKE KUCHAGUA MWENZA (MCHUMBA) INACHEKESHA SANA, SOMA ZAIDI HAPA
Wanasaikolojia wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones wamegundua kwamba, mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume ambaye angependa kuwa rafiki au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata wanawake wenzie wanampenda kama yeye anavyompenda……..
Anavyozidi kuwaona wanawake wenzie wakitabasamu au kumchekea mwanaume huyo anapopita mbele yao ndivyo atakavyojua kwamba, huyo mwanaume ni mzuri.
Hali hii inafahamika kama copycat reflex na ni matokeo ya nadharia ya Darwin ya mambo ya mabadiliko ya maumbile ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu hao, yaweza kutumika pale ambapo mwanamke anakumbana na wanaume wengi wanaomtaka lakini anapata matatizo ya kumchagua yupi na kumwacha yupi.
Au akiona uchaguzi wa mwanaume bora utamchukulia muda wake mwingi na nguvu zake hujirahisishia kwa kuchukua uamuzi wa kuwaangalia wanawake wenzie wanavyomwona mchumba wake mtarajiwa.
Uchunguzi huu hufanyika bila wanawake wenzie kujua kwa hiyo mwanaume anayeonekana kuchangamkiwa sana na wanawake wenzake kwa lengo la kumvuta ili awe mpenzi wake ndiye ambaye atapata uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na mwanamke huyo.