Friday 20 March 2015

MWANAMKE FAHAMU NJIA KUU KUMI (10) ZA KUMFANYA MWANAUME AONGEZE MAPENZI NA KUKUHESHIMU

Image result for MWANAMKE AMEVAA KIHESHIMA


1. Vaa vizuri (look sexy) pindi unapokuwa nae hii itamfanya aendelee kukuona mpya kila siku.

2. Jiheshimu, mwanamke unapokuwa unajiheshimu hata mwanaume pia hukuheshimu na haitakiwi ujirahisishe pindi unapokuwa nae jua thamani yako kama mwanamke.

3. Tumia muda wako na marafiki zako au kukamilisha malengo yako binafsi. Hii itafanya mwanaume akukumbuke sana pindi unapokuwa haupo na kukupigia simu mara kwa mara.
Image result for MWANAMKE AMEVAA KIHESHIMA
4. Kuwa na maisha yako usimtegemee mwanaume kwa asilimia 100, hii itamfanya asikukandamize kwa kujua bila yeye wewe huwezi kusimama, mtegemee
pale tu unapozidiwa.

5. Uwe mbunifu kitandani, hii itamfanya mwanaume akukumbuke kwa utashi wako na kumfanya asijisikie kutoka nje ya mahusiano, usiwe gogo utaboa.

6. Kuwa mwanamke makini hasa kwa kujihusisha na vitu mbalimbali vya kijamii na taharifa mbalimbali zinazoihusu jamii visikupite ili kuendana na dunia ya sasa.


7. Jitume sana katika kazi hasa wakati anapokuchukulia poa. Kamwe usimpe nafasi mwanaume wako akuone kama wewe wa ziada kwake jitume kiasi kwamba awe anakuogopa.

Image result for MWANAMKE AKIMSIFIA MME WAKA

8. Jenga mazingira ya kuonyesha kwamba unamkubali mbele ya kadamnasi hii itamfanya ajione mwenye bahati kuwa na wewe.

9. Muepuke pindi anapokukosea heshima usijibizane nae na pia usijibu “message” wala kupokea simu
kama adhabu na pia kupunguza hasira, hii itasaidia kwa yeye kujirekebisha.

10. Fata ndoto zako mwenyewe, kuwa mvumilivu kuhusu maisha na malengo yako. Ukiwa ni mtu wa
kubadilika badilika, hueleweki na wala hujui usimame upande gani mwanaume atashindwa kukuheshimu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA