ALIYEKUWA MHARIRI WA KAMPUNI YA MWANAHALISI, EDSON KAMUKARA KIJIJINI AZIKWA BUKOBA
Pacha wa Marehemu Edson(kushoto) Dada Edda na Kulia ni Dada yao Jeniffer kwenye masikitiko makubwa ya Kuondokewa na Ndugu yao.
Katikati ni Dada Joyce akiwa na baadhi ya Wanafamilia
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea(kulia) akifafanua jambo na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania
Daima. Picha na Faustine Ruta.
Sehemu ya Wanakwaya wakiendelea kuimba nyimbo
Pacha wa Marehemu(kushoto) kwa machungu akiangalia Picha ya Ndugu yake wakati wa Kumuaga kuelekea nyumba yake ya Milele leo jumatatu juni 29, 2015. Picha na Faustine Ruta
Viongozi wa Dini wakitoa salaam zao za mwisho
KWA PICHA ZAIDI SOMA HAPA CHINI

Kulia ni Mkurugenzi wa Radio Kasibante Fm 88.5 nae alikuwepo na hapa akitoa salaam zake za mwisho
Dada yake mkubwa na marehemu Joyce akisoma kwa ufupi historia ya Marehemu Mdogo wake Edson Salvatory Kamukara, Picha na Faustine Ruta
Mwandishi
mkongwe na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania
Daima akitoa neno kuhusu msiba huo wa Mhariri Marehemu Edson S. Kamukara
leo wakati wa Kumuaga rasmi Kijijini kwao Muleba kusini.
Umati mkubwa wa Watu walijitokeza kumuaga
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea akitoa neno kuhusu Msiba huo wa
Kijana aliyekuwa Mpiganaji kupitia Kampuni hiyo. Kubenea ameweka wazi kuwa Mtoto aliyeachwa na Marehemu kampuni yake itaendelea kuwa karibu nae kimsaada zaidi.
Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno kwa Niaba ya waandishi wa Habari Kagera waliojumuika pamoja katika sehemu hiyo kuuaga mwili wa mwenzao Edson Salvatory Kamukara, Picha na Faustine Ruta

Pacha wa Marehemu akisikitika kuondokewa na mwenzie waliozaliwa pamoja
Dada wa marehemu Edson akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara. Picha na Faustine Ruta

Edda Pacha wa Marehemu akiwa kwenye huzuni kubwa




0 comments:
Post a Comment