Friday 31 July 2015

CCM ZANZIBAR YATOA TAMKO KUHUSU KUHAMA KWA LOWASSA

unnamed (4)
Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga akitoa taarifa ya Chama hicho kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa ndani ya Chama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa katika mkutano uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
unnamed (5)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
unnamed (6)
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar.(VICTOR)

2
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni Chama kikubwa chenye wafuasi na wanachama wengi pamoja na Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na uadilifu mkubwa.
Hayo yameelezwa na Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na Chama cha upinzani huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Amesema CCM ni Chama kinacho aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa Tanzania hivyo kujitoa kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama haiwezi kukiathiri chama hicho.
Nyawenga ameongeza kuwa wingi wa wanachama wa chama hicho haujaletwa na utajiri wa vingozi wake bali umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi yake.
Alisema CCM haina hasara kumpoteza mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na itikadi ya Chama kwa maslahi yake binafsi na marafiki zake hata kama utajiri wake ni mkubwa wa kupindukia.
Ameongeza kuwa uwamuzi wa Lowassa kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la kukishituwa chama, viongozi, pamoja na wanachama wake na hakiwezi kudhoofika wala kutetereka.
Alisema hii sio mara ya kwanzi kwa Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi mwandamizi na kujiunga na vyama vya upinzani na bado kinaendelea kuimarika.
“Mwaka 1989, CCM iliwafukuza uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino Lyatonga Mrema na mwaka jana CCM ilimfukuza uanachama aliyekua Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,” alikumbusha Katibu wa Chama Mkoa.
Nyawenga aliweka wazi kuwa umaarufu alionao Lowassa inawezekana umejengwa kutokana na CCM lakini haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa kutokana na yeye.
Alisema wanachama wa Zanzibar waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani ya Chama na sasa baada ya kuhama wameamua kujitenga na hawako pamoja naye.
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib Borafia Silima amesema kwamba Tanzania inaheshimika kuwa ni nchi yeye amani, na mshikamano na Chama cha Mapinduzi kinafuata utaratibu wa katiba iliyowekwa.
Amesema kila Mwanachama anayo haki na uhuru wa kuchaguwa kiongozi anayemtaka na yeye kuchaguliwa na mtu yeyote ikiwa ni Demokrasia iliyotandikwa na Chama hicho.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA