Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Sunday, 16 January 2022

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Akiongoza kikao (Maalum) cha kamati Maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo Jumapili tarehe 16 Januari, 2022 Afisi Kuu CCM Kisiwandui.

  

Wajumbe wakifuatilia Baadhi ya Nyaraka za Kikao Hicho.

Tuesday, 26 September 2017

RUTAINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA



NA BASHIR NKOROMO
Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.

Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa  katika uchaguzi wa awali.

Wakati katika awamu ya kwanza  Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.

Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181. PICHA ZA UCHAGUZI HUO/>BOFYA HAPA

Monday, 25 September 2017

NASSARI AWEKA UBUNGE REHANI SAKATA LA MADIWANI ARUSHA KUHAMIA CCM

Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge wake  baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais.

Nassari amedai ana ushahidi wa kielektroniki unaoonyesha madiwani hao walivyopewa rushwa ili wajiuzulu nafasi zao.

Hata hivyo, diwani wa Kata ya Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi ambaye amepokewa na Rais Magufuli juzi  baada ya kujiuzulu Chadema akizungumzia tuhuma hizo alisema madai hayo hayana ukweli wowote na kama Nassari ana ushahidi ni vyema angeutoa hadharani.

Ngowi aliwashauri Chadema mkoani Arusha watatue matatizo yaliyopo ndani ya chama hicho na wasitafute visingizio kwa kuwa yeye ameamua kujiuzulu kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na hajapewa rushwa yoyote.

Diwani mwingine aliyejiengua katika chama hicho wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe alisema hakuna chochote alichopewa kama rushwa kwa lengo la kujiuzulu, akimshauri Nassari autoe hadharani ushahidi anaousema na si kushusha tuhuma zisizo na mashiko.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Nassari alisema ushahidi huo ameuhifadhi ndani ya ‘flash disc’ na yuko tayari kumkabidhi Rais Magufuli na vyombo vya uchunguzi.

Mbunge huyo alisema endapo ikithibitika kuwa ushahidi wake ni wa uongo yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.

“Ninao ushahidi na kama Mheshimiwa Rais yuko tayari niko tayari kumpatia ninayo flash, ushahidi ninao kwa muda mrefu na tulijua watapokelewa juzi madiwani wawili lakini mmoja amekataa akaenda mmoja,” alisema Nassari. 
 
Alidai kwamba  kwa kipindi kirefu alipokuwa masomoni nchini Uingereza alikuwa akijiuliza ni kwa nini madiwani katika Mkoa wa Arusha wamekuwa wakijiuzulu na ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa kina.

Nassari akiwa ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika mkutano huo, alisema alianza kufanya uchunguzi Mei kwa kutumia vifaa vya kielektroniki alivyovinunua nchini Uingereza na kubaini kwamba baadhi ya madiwani wanaojiuzulu walipewa rushwa ya fedha, ahadi ya vyeo na ya makazi.

Alisema uchunguzi juu ya tuhuma za madiwani hao kujiuzulu aliufanyia ndani ya ofisi ya umma akisisitiza hakuna diwani wa Chadema mkoani Arusha ambaye amejiuzulu kwa kumuunga mkono Rais Magufuli bali wamepewa rushwa.

“Mheshimiwa Rais anapambana na rushwa lakini kuondoka kwa madiwani ni mfumo wa rushwa anaopambana nao niko tayari kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge endapo ikithibitika ushahidi wangu ni wa uongo,” alisema Nassari.

Madiwani wapatao 10 wa Chadema wamejiuzulu kwa nyakati tofauti. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ameshawahi kunukuliwa akikanusha tuhuma za kupewa rushwa madiwani wanaojiengua kutoka Chadema na kujiunga na CCM.

Polepole Julai alikaririwa akisema iwapo Chadema ina viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi ni chama cha  ovyo kwa kuwa chama kilicho imara na watu wake wapo safi hawawezi kuhongeka.

Alitoa kauli hiyo mjini Bagamoyo alipohudhuria mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso) Mkoa wa Pwani.

RAIS MAGUFULI KUONGOZA VIKAO VYA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA - NEC JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017.

Kwa mujibu wa  taarifa iliyotolewa jana  Septemba 24 na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ameeleza kuwa, Kamati kuu ya Halmashauri ya Taifa (CC)  na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia kuketi  Jijini Dar e Salaam kwa nyakati tofauti.

Friday, 1 September 2017

ODINGA: NI SIKU YA KIHISTORIA KENYA NA KWA AFRIKA

Image result for uchaguzi kenya 2017
Picha / Maktaba
Uchaguzi
Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.
Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.
Imetoa mfano mwema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Image result for Kalonzo Musyoka
Naye Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka amesema mahakama imekuwa mfano mwema kwa Afrika na dunia nzima.
"Ninajivunia kuwa Mkenya leo," amesema.
"Sasa tutaangalia kina kuhusu tume ya uchaguzi. Hatuan imani kwamba wanaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki."

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KUU YA KENYA YAAMURU UCHAGUZI MKUU WA KENYA URUDIWE BAADA YA SIKU 60

Image result for uchaguzi kenya 2017


Image result for uchaguzi kenya 2017




















MAHAKAMA Kuu nchini Kenya, imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Raila Odinga, urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.

Mahakama Kuu ya Kenya, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufiuatia maombi ya Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8, 2017 na kumpa ushindi Rais Kenyatta.

Katika maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa kwa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matokeo.


Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

Tuesday, 22 August 2017

NEC YATEUWA MADIWANI 12 WANAWAKE WA VITI MAALUM

Kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika  tarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12) kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
 
Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

NA.JINACHAMAHALMASHAURI
  1. 1
Ndugu Saida Idrisa KiliulaCUFHalmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Ndugu Sophia Charokiwa MsangiCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mwanga

Ndugu Shahara Selemani NduvaruvaCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Ndugu Neema K. NyangaliloCCMHalmashauri ya Manispaa ya Ilala

Ndugu Farida Zaharani MohamedCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mvomero

Ndugu Lucia Silanda KadimuCCMHalmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)

Ndugu Amina Ramshi MbairaCCMHalmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

Ndugu Janeth John KaayaCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Meru

Ndugu Sara Abdallah KatangaCHADEMAHalmashauri ya Manispaa ya Ilala

Ndugu Ikunda MassaweCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Hai

Ndugu Tumaini Wilson MasakiCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Siha

Ndugu Elizaberth Andrea BayyoCHADEMAHalmashauri ya Mji wa Mbulu

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.
 
Imetolewa  tarehe 21 Agosti, 2017
Kailima, R. K
 
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Monday, 21 August 2017

KATIBU WA CCM MKOANI SINGIDA AMPONGEZA DC IKUNGI

BMG Habari, Pamoja Daima!
Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Singida kimempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani humo Mhe.Miraji Mtaturu kwa kuanzisha michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 ili kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia utatuzi wa changamoto za elimu kupitia Mfuko wa Elimu Ikungi.

Katibu wa chama hicho mkoani Singida, Jimson Mhagama (pichani) alitoa pongezi hizo jana Agosti 19,2017 kwenye uzinduzi wa michuano hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Ikungi mkoani Singida ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.

Uzinduzi wa michuano hiyo, ulikwenda sambamba na uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara uliokwama tangu mwaka 2009 katika shule ya sekondari Ikungi hii ikiwa ni uzinduzi rasmi wa zoezi kama hilo kwenye kata zote wilayani Ikungi ambapo kila Kata imepewa jukumu la kufyatua matofali elfu kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.

Katika zoezi hilo, walijitokeza wadau pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wenyeviti wa halmashauri, jeshi la polisi, Tanesco na wanachi ambao walimuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Mtaturu aliyekabidhi mifuko 100 ya simenti na wao wakachangia fedha taslimu zaidi ya shilingi 800,000 na ahadi zaidi ya shilingi 1,900,000, ahadi za simenti mifuko 194 na mchanga wa moramu malori matano kutoka kwa mdau wa maendeleo wilayani Ikungi Hussein Sungita.

Thursday, 17 August 2017

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI TENA OMBI LA WABUNGE 8 WA CUF WALIOSIMAMISHWA NA LIPUMBA

Wabunge wanane waliofukuzwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Prof Ibrahim Lipumba, jana waliondoka vichwa chini baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kutupilia mbali ombi lao la zuio la kupinga kuapishwa kwa wabunge wapya.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Lugano Mwandambo baada ya kusikiliza hoja zote za pande mbili, ambapo amesema kuwa mahakama imetupilia mbali hoja za walalamikaji za kuweka pingamizi kutaka wabunge wapya wasiapishwe mpaka kesi ya msingi isikilizwe.

Aidha, Mwandambo amesema kuwa mahakama itasikiliza pingamizi la walalamikaji walilofungua kupinga kufukuzwa uanachama wa chama cha wananchi CUF na mwenykiti wao Prof. Ibrahim Lipumba.

Katika maombi yao walalamikaji wanaomba kutoapishwa kwa wabunge wanane walioteuliwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao kwa mujibu wa katiba.

Wednesday, 16 August 2017

UMOJA WA MATAIFA WAKATAA OMBI LA RAILA ODINGA

Afisa wa Umoja wa Mataifa, amekataa ombi la kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga la kutaka umoja huo kufanya tathmini mpya ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, ameunga mkono kauli ya Katibu Mkuu, Antonio Gutrres, ya kuwataka wanasiasa wa Kenya wanaopinga matokeo ya uchaguzi kufikisha masuala hayo mbele ya taasisi zenye mamlaka ya kutoa maamuzi Kikatiba.

Bw. Haq amesema, Umoja huo utafuatilia kauli za Bw. Odinga kuhusu uchaguzi mkuu huku gazeti la Washington Post likisema uchaguzi wa Kenya ulikuwa huru na wa haki.

Saturday, 12 August 2017

UHURU KENYATTA ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYA

Tume huru ya uchaguzi Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne akipata kura 8,203,290.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amekabidhi cheti cha ushindi kwa Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.

Akihutubia jana mara baada yakutangazwa kuwa mshindi, Rais Kenyatta amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.

“Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Kenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” alisema.

“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”

Kwa upinzani alisema: “Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu.”

“Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja.”

“Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”

Katika takwimu
  • Bw Kenyatta alipata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zilizopigwa
  • Bw Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote zilizopigwa
  • Waliojitokeza walikuwa 15,073,662 ambayo ni asilimia 78.91 kati ya 19m waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura
  • Siku ya Alhamisi upinzani ulidai  kwamba Raila Odinga alishinda uchaguzi na kuitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais

Friday, 4 August 2017

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA WABUNGE 8 WALIOFUKUZWA CUF

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa  Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.

Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

Thursday, 27 July 2017

KAULI YA ZITTO KABWE BAADA YA KUITWA MSALITI KUFUATIA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI

 Na Regina Mkonde

 Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewajibu baadhi ya watu wanaomkosoa na kumuita msaliti kutokana na kitendo cha kumsifia Rais John Magufuli alipokuwa ziarani jimboni humo.

Zitto alijibu mapigo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kigoma Mjini, ambapo alisema asingeweza kumkosoa Rais Magufuli wakati ule kwa kuwa alikuwa mgeni jimboni kwake, pia alikuwa anafanya shughuli za maendeleo ya wananchi wa jimboni kwake.

“Rais alikuja hapa akafungua mradi wa maji tukaenda ziwa Tanganyika, kuna watu walikasirika sababu Rais alinisifia sana, hawezi akaja Kigoma mtu akanisema mimi vibaya msingekubali, na mgeni akija siwezi nikaanza kumsema vibaya, mgeni akija unamkaribisha anafanya kazi yake anaondoka, kwani rais akienda kwenye majimbo yao wanamsema, rais alikwenda Bukoba Mjini wakati wa tetemeko, mbunge wa jimbo hilo alimsema ? alikwenda Arumeru kwa mdogo wangu Joshua Nasari, alimsema rais kwa nini akija kigoma mimi ndio nimseme,” alihoji Zitto.

Aliongeza kuwa “Mimi hamkunifundisha kuwa mazwazwa wazee mlinifundisha adabu na kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini sio kwamba rais akikosea hatutamsema tutamsema, na tumeshamsema sana, sisi ndio chama cha mwisho kufanya mkutano wa ziara, tukaja operesheni ya linda demokrasia tumemaliza mikutano ikapigwa marufuku.”

“Lakini toka serikali ya awamu ya tano iingie madarakani uhuru umeanza kuminywa sasa ni lazima, hatuwezi kukaa kimya haki ya watu kuwa na mawazo tofauti hatuwezi kuikalia kimya hata kidogo, lakini wakati huo huo hatuwezi tukasimamisha kila kitu kusubiri haki ya kuwa na mawazo huru, lazima haki ya mawazo huru ipiganiwe wakati tunapigania maendeleo,” amesema

BUNGE LARIDHIA KUVULIWA UANACHAMA WABUNGE 8 WA CUF

Image result for bunge la tanzania 2017
Siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na Madiwani wawili, Bunge limeridhia.

Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.

MADIWANI 3 WA CHADEMA WAJIUZULU NA KUJIUNGA CCM

Wakati Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kutimka kwa kile wanachodai kuwa ni kuweza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Mapema leo mchana Julai 26, 2017, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM.

Madiwani waliojiuzulu ni, Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na  Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati.

Akizungumza wakati wa kutangaza azma hiyo, Goodluck Kimaro alisema kwamba CHADEMA hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu. 

Akitolea mfano Halimashauri ya Wilaya ya Hai ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni Mbunge wa jimbo hilo, alisema chama hakina uwezo wa kufanya jambo lolote dhidi ya mbunge.

Endapo mbunge atashindwa kutekeleza majukumu yake, chama ndio kinatakiwa kumuadhibu, lakini kwa upande wetu wa Hai hakuna uongozi wa kuweza kufanya hivyo. 

Mbunge huwa hafanyi ziara za kutembelea jimbo kama anavyotakiwa, lakini bado chama hakina sauti, alisema Goodluck Kimaro.

Baada ya madiwani wote kuzungumza, Polepole alionya juu ya uwepo wa vitendo vya kihalifu kwa madiwani ambao wanahama CHADEMA na kusema jambo lolote likitokea kwa madiwani hao waliohama, watashughulikiwa ipasavyo na vyombo vya dola lakini pia chama hicho kingine ndio watakuwa wahusika.

Hadi sasa jumla ya madiwani 9 mkoani Arusha tayari wamejiunga na CCM na sasa watatu mkoani Kilimanjaro nao wamejiunga.

Wednesday, 7 June 2017

MSAJILI WA VYAMA AZUNGUMZIA SAKATA LA MAALIM SEIF KUFUNGUA OFISI MPYA ZA CUF


Kutokana na Chama cha Wananchi (CUF) kufungua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa Kata ya Mzimuni, Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Msajili wa Vyama vya Siasa amesema anaamini chama hicho kinafanya mambo yake kwa kuzingatia sheria.

Jana  Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alisema hajapata taarifa yoyote ya chama hicho, kufungua ofisi mpya zaidi ya kuona katika vyombo vya habari.

“Ukiondoa taarifa za kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo (jana), lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta taarifa, “ alisema Jaji Mutungi.
IMG_7380.JPG
Jaji Mutungi alisema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo. 

Upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad wamefungua ofisi hizo, baada ya tukio la kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba.

Jaji Mutungi alisema atakapopokea taarifa rasmi ataangalia kama taratibu zilifuatwa kwani ufunguaji wa ofisi mpya una taratibu zake. 

“Nikiletewa taarifa ndio nitajua kama walifata taratibu au la, ufunguaji wa ofisi una taratibu zake najua wanazijua pia, “ alisema Jaji Mutungi.

Alisema taarifa hiyo ataipata kutoka kwa mwenyekiti au msemaji wa chama, ambaye ni katibu mkuu ambao wanatambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa. 

Akizindua ofisi hiyo Juni 4 mwaka huu, Maalim Seif alisema ofisi hiyo imetolewa na wabunge 40 wa CUF.

Alisema uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni kitendo cha kiungwana na kiungwe mkono na wanachama wote. 

Alisema kwa miezi 10 sasa, wamekuwa wakishindwa kufanya kazi kwa upande wa Tanzania Bara, jambo ambalo limewaathiri hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu bila hofu yoyote.

Katibu huyo alisema ana imani na mahakama kuwa itawapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Sunday, 2 April 2017

MAHAKAMA KUU YAMWAMURU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOTOA RUZUKU KWA PROF. LIPUMBA NA KUNDI LAKE MPAKA SHAURI LITAKAPOAMULIWA

Image result for law

Mahakama Kuu imemuamuru Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutotoa ruzuku kwa Prof. Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi, CUF, na kundi lake.

Zuio hilo ni mpaka shauri dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Uamuzi huo umefikiwa na Jaji Dyansobela baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa kwa hati ya dharura.

Jopo la Mawakili wa CUF, liliiomba Mahakama Kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali shilingi milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa chama kuhusu fedha hizo ikizingatiwa kwamba, Prof. Lipumba alishavuliwa uanachama.

Mawakili hao akiwemo Juma Nassor , wamesisitiza kwamba, mazingira yaliyopo ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia serikalini.

Aidha, wameiomba Mahakama Kuu kwamba amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya msajili kumtambua Prof Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa rufani ya kufanyiwa marejeo mbele ya Mahakama ya Rufani Tanzania.

Monday, 27 March 2017

CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA 31, WA WILAYA 155,YAELEZA MSIMAMO WA CHAMA KUHUSU MAKONDA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya uongozi, muundo na mfumo, kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 31 wakiwamo wapya 20, na wa wilaya 155 ambao uteuzi wao unaanza mara moja kuanzia jana.

Pia chama hicho kimekiri kufanya mabadiliko ya kikatiba yanayolenga maeneo matatu ambayo ni misingi ya uongozi, muundo na mfumo pamoja na utawala na utendaji kwa lengo la kukijenga zaidi chama hicho, na hakuna sehemu yoyote kwenye Katiba hiyo iliyobadilishwa inayohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema kati ya makatibu hao walioteuliwa wa mikoa 11 ni wale waliopandishwa hadhi kutokana na utendaji wao na 20 ni wapya kabisa.

Alisema katika orodha ya makatibu hao walioteuliwa, chama hicho kilizingatia sifa hizo ikiwemo maadili, weledi, jinsia na mpango wa kuachiana vijiti kwa kuzingatia rika.
 
Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa…
  1.     Arusha- ­ Elias Mpanda
  2.     Dar es Salaam-­ Saad Kusilawe
  3.     Dodoma- ­ Jamila Yusuf
  4.     Geita- ­ Adam Ngalawa
  5.     Iringa- ­ Christopher Magala
  6.     Kagera­- Rahel Degeleke
  7.     Katavi­- Kajoro Vyahoroka
  8.     Kigoma-­ Naomi Kapambala
  9.     Kilimanjaro-­ Jonathan Mabihya
  10.     Lindi­- Mwanamasoud Pazi
  11.     Manyara- ­Paza Mwamlima
  12.     Mara- ­Innocent Nanzabar
  13.     Mbeya- ­Wilson Nkhambaku
  14.     Morogoro-­ Kulwa Milonge
  15.     Mtwara- ­Zacharia Mwansasu
  16.     Mwanza-­ Raymond Mwangala
  17.     Njombe-­ Hossea Mpagike
  18.     Pwani-­ Anastanzia Amasi
  19.     Rukwa-­ Loth Ole Nesere
  20.     Ruvuma­- Amina Imbo
  21.     Shinyanga- ­Haula Kachambwa
  22.     Simiyu-­ Donald Etamya
  23.     Singida-­ Jimson Mhagama
  24.     Tabora-­ Janeth Kayanda
  25.     Tanga-­ Allan Kingazi.
“Makatibu wengi (20) tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra” amesema Polepole.

Lakini pia alisema katika orodha hiyo ya makatibu wa wilaya wa CCM 155, makatibu 76 ni wapya kutokana na vigezo vipya vilivyowekwa na chama hicho.

Aliwataja baadhi yao kuwa ni Mussa Matoroka anayekwenda Arumeru, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gaddafi’ (Longido), Joyce Mwenda (Namtumbo), Kombo Kamote (Bagamoyo), Grevas Ndaki (Momba), Othman Dunga (Hanang), Pili Augustino (Dodoma Mjini) na Martin Mwakitabu (Chamwino).

Wengine ni Aveline Ngwada (Bukombe), Nuru Ngeleja (Chato), Michael Mbaga (Iringa Mjini), Afidu Luambano (Temeke), Joyce Mkaugala (Ilala), Hanaf Msabaha (Kinondoni), Salum Kali (Ubungo), Robert Kalenge (Kigamboni), Ramadhan Dallo (Arusha) na Gulisha Mvanga (Monduli).

Kuhusu suala la Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Polepole alisema, kwanza napenda kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria’… CCM inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza. Lakini pili, Mkuu wa Mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu, hivyo badala ya kukaa na kumpangia Rais kitu cha kufanya, tumuache afanye kazi’.. “

Aidha, Humphrey Polepole akitolea ufafanuzi madai yanayoenezwa kuwa wamefanya mabadiliko kuwa Rais Magufuli ndiye atakayegombea 2020 bila kupingwa amesema kuwa, mabadiliko ya katiba waliyoyafanya katika mkutano mkuu maalum, hayakuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa uchaguzi mwaka 2020. Hivyo tunawaomba wanachama wetu na watanzania wapuuze habari nyingine zinazoenezwa.

Katibu wa CCM itikadi na Uenezi ­Taifa

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA