Sunday 10 July 2016

HAPANA CHEZEA KIFO:::FISI AJIFICHA NDANI YA MZOGA KUYAOKOA MAISHA YAKE

Habari Mdau wa Funguka Live ,leo nimeona tujikumbushe kisa hiki cha kusisimua sana ambapo ni nadra sana kupatikana , nimatumaini yangu utafurahi na kujifunza kitu.
 Na  Stratton Hatfield

Katika kujiokoa kwenye hatari yeyote ile si tu watu ambao wanaweza kupata wazo la ajabu la kutenda ilimradi tu kuepukana na mauti, fisi mmoja aliyekuwa katika lishe yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimika kujificha kwenye tumbo la mzogo wa tembo ili kumkwepa simba dume aliyemvamia ghafla.

Fisi huyo aliyaona mauti yaleeeeee, lakini aliona ni heri kukaa ndani ya tumbo la tembo kulikoni kuliwa na simba. picha zifuatazo zinaonyesha namna fisi huyo alivyojificha na baadae kufanikiwa kukimbia baada ya kupata upenyo.

Tukio hilo halijatokea mbali bali ni kule Masai Mara, pata uhondo huo.


Simba akiwa katika doria kumsubiri mtuhumiwa wake ambaye naye aliendelea kujichimbia mafichoni humo
Taswira ya fisi ndani ya mzoga
  

Hali ilipokuwa shwari alichomoka kwa mwendo kasi
Simba akiendelea kumfukuza mtuhumiwa wake hata baada ya kuchomoka mafichono


Photo Credit ::Hatfield & Klaassen

    0 comments:

    Post a Comment

    OFFICIAL MEMBER

    OFFICIAL MEMBER

    Please Share This Site

    HABARI ZETU

    LIKE PAGE YETU HAPA