Sunday 16 August 2015

HIVI NDIVYO FAINALI YA KINONDONI TALENT SEARCH ILIVYOFANA

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Wasanii, Simon Mwakifamba.
Mshindi kwa upande wa wachekeshaji, Nurdin Bakari 'Balotelli' akitoa kichekesho mbele ya Rais KIikwete.
Mmoja wa washiriki akiimba.
Mpoki (wa pili kutoka kulia) akiwa na washindi wa Kinondoni Talent Search. (P.T)

Balotelli (katikati) akilia kwa kutoamini mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kuchekesha.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumzia shindano hilo mbele ya washiriki walioingia fainali.
Msanii wa Bongo Fleva, Baranaba akitoa burudani katika shindano hilo.
Msanii wa Hip Hop, Fid Q akitoa michano katika shindano hilo.
 
Mmoja wa washiriki kwa upande wa kucheza, akionesha kipaji chake.
Msanii wa filamu Bongo, Jacob Steven 'JB' akiwa na Richie Richie (kushoto nyuma).
Mtangazaji, Mboni Masimba (kulia) naye alikuwepo katika shindano hilo.
Wasanii wa Bongo Fleva, Shilole na Nuhu Mziwanda wakifuatilia shindano hilo.
Wasanii wa kuchekesha kutoka Kundi la Mizengwe wakiwa katika pozi.
 
Msanii kutoka Bongo Movie, Vicent Kigosi 'Ray' akifanyiwa mahojiano red carpet. 
Msanii wa Bongo Fleva, Pipi Doreen akiingia kwenye shindano hilo.
JANA ndani ya Ukumbi wa Kisanga, Kijitonyama jijini Dar, ilikuwa ni siku maalum ya kilele cha shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Kinondoni Talent Search ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Katika shindano hilo lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda lilikuwa la aina yake kutokana na mshereheshaji ‘MC’ Mpoki kutoka Orijino Komedi kumchekesha vilivyo Rais Kikwete.
 
Wakati wa kufungua pazia la burudani, Paul Makonda alianza kwa kutoa shukrani kwa Rais Kikwete kwa kuhakikisha ameiweka sanaa sehemu nzuri kabla ya kumaliza kipindi chake.
“Tunamshukuru Rais Kikwete kwa uwepo wake hapa kama mgeni rasmi. Pia uwepo wake hapa umeonesha ni jinsi gani anaithamini sanaa yetu. Ni dhahiri ameifikisha mbali na kila kijana anaiona kama ni sehemu ya ajira,” anasema Makonda.
Ikumbukwe pia katika Ukumbi wa Mlimani City, Kikwete aliongea na wasanii na kueleza jinsi sanaa alivyoiweka pazuri na kuwahakikishia hata akimaliza muda wake bado ataendelea kuwa mlezi wa wasanii wote nchini na kuwafungulia milango kufika mbali zaidi.
SHINDANO
Mwishoni mwa mwezi Machi, mwaka huu, Makonda alianzisha Shindano la Kinondoni Talent Search likiwa na lengo la kuwapa fursa vijana wengi kuweza kuonesha vipaji vyao na kujipatia ajira moja kwa moja kupitia vipaji hivyo.
Katika mchujo uliofanyika katika Fukwe za Coco, vijana zaidi ya 100 walijitokeza na kuchujwa.
“Safari ilikuwa ndefu sana, leo hii (Jana Jumamosi) fainali tumebakiwa na washiriki kumi na tano ambapo wamegawanya katika makundi matatu yaani kuimba, kucheza na kuchekesha,” anasema Makonda.

Kucheza
Katika fainali hizo washindi watatu waliibuka kidedea ambapo kwa upande wa kucheza, Laidanus Vitalis alijipatia shilingi milioni tano na ofa maalum ya kufundishwa kucheza bure mwezi mzima sambamba na chochote atakachokitaka kupitia kipaji chake ndani ya mwaka mmoja.
Kuimba
Kwa upande wa kuimba, Lilian Michael aliibuka mshindi na kujipatia kitita cha shilingi milioni tano sambamba na kurekodi studio yoyote iliopo Kinondoni na kupewa fursa nyimbo zake kuchezwa bure ndani ya mwaka mmoja.
Kuchekesha
Nurdin Bakari ‘Balotelli’ naye aliibuka kidedea kwa upande wa kuchekesha na kufanya ukumbi ulipukwe kwa shangwe. Ushindi huo umemuwezesha naye kujizolea shilingi milioni tano sambamba na kupata fursa ya kukitangaza kipaji chake bure ndani ya mwaka mmoja.
Mastaa 
Shindano hilo lilifunikwa na mastaa kibao katika tasnia ya filamu na muziki kama vile Shilole, Wema, Mirror, Monalisa, Baby J, Izzo B, Pah One, Natasha, JB, Richie, Odama, Rose Ndauka na wengine kibao.
Baadhi ya mastaa waliotoa burudani kusindikiza shindano hilo ni Barnaba, Ruby na Fid Q.
(STORI/PICHA: ANDREW CARLOS NA MUSA MATEJA)

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA