Monday 17 August 2015

YANGA YAICHANGAMSHA MBEYA CITY MECHI YA KIRAFIKI

11863434_732791986867181_7612666654763943644_n
Miamba ya kandanda Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans imeendelea kuinyanyasa Mbeya City FC baada ya jioni ya jana kuichapa 3-2 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.Magoli ya Yanga yamefungwa na Mbrazil, Andrey Coutinho, Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma, wakati magoli ya Mbeya City yamefungwa na Bakari Mwinjuma na Meshack Samuel.
Hiki ni kipigo cha tatu cha aina hiyo kwani msimu uliopita katika mechi mbili za ligi kuu, Yanga ilishinda 3-1 uwanja wa Taifa na ikapata ushindi kama huo uwanja wa Sokoine.
Msimu wa 2013/2014 ambao Mbeya City waliishia nafasi ya tatu walitoka sare ya 1-1 uwanja wa Sokoine na wakafungwa 1-0 uwanja wa Taifa.
Kwa lugha rahisi, Mbeya City wanaendelea kuwa wateja wa Yanga iwe mechi za mashindano au kirafiki.(

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA