Friday, 21 August 2015

KASEJA RASMI MBEYA CITY

Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa Agosti 19, 2015 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo na kumaliza maswali ya kuwa angecheza wapi msimu ujao.
Taarifa hizi huenda ni pigo kwa kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa anahitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City, Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya Yanga na kufanya kesi hiyo kutinga mahakamani

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA