MSENEGAL WA SIMBA ATUA DAR TAYARI KWA KAZI TA LIGI KUU BARA
Simba iko katika hatua za mwisho kumalizana na mshambuliaji hatari kutoka Senegal ambaye anatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili zijazo.
Mshambuliaji Papa Niang, raia wa Senegal aliyezaliwa Desemba 5, 1988, sasa ana miaka 26 ametua jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Niang ambaye inaelezwa ni mdogo wa Mamadou Niang, ametua jijini Dar es Salaam kumalizana na Simba na mara moja kuanza kazi.
Akizungumza na SALEHJEMBE mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Niang amesema yuko tayari kufanya kazi.
“Nimekuja nikiwa tayari, inategemea makubaliano yangu na klabu hii yatakuwaje,” alisema.
Taarifa zinaeleza kwamba kabla ya kumsajili, Simba itampa nafasi ya mazoezi ya siku tatu, pia ataichezea katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mwadui FC.
-SALEH JEMBE
0 comments:
Post a Comment