UTOAJI MIMBA HOLELA WAONGOZA KWA VIFO NCHINI KULIKO UGONJWA WA SARATANI
Utoaji mimba holela umeongezeka nchini Kenya, ambapo watoaji mimba wasionasifa husababisha vifo vya wanawake 2,600 kila mwaka idadi ambayo ni kubwa kuliko hata ya vifo vitokanavyo na saratani ya shingo ya uzazi nchini humo.
Wizara ya Afya ya Kenya imesema karibu matukio laki tano yautoaji mimba hufanywa nchini Kenya kila mwaka, ambapo kati ya hayo 375,000 hufanyika vichochoroni.
Timu ya Wataalam wa Afya ikiongozwa Joyce Mumah wa Shirika la Utafiti la Idadi ya Watu Afrika (APHRC), imesema watoaji mimba wasionasifa sio tu huuwa wanawake 2,600 pia huwaachia majeraha ya kudumu.
Mwaka jana wanawake 2,451 nchini Kenya walikufa kwa saratani ya shingo ya uzazi kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
0 comments:
Post a Comment