Wednesday 25 November 2015

PROF. MWANGAMILA ALIONDOKA ,AMINA SANANI AMETANGULIA NI UAMUZI WA ALLAH


Mwandishi Kiduo Mgunga
Ni miezi imepita tangu Prof.Mwangamila atangulie mbele za haki.Ulikuwa wakati mgumu sana  na ilichukua muda huzuni kunitoka ila kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti kifo chake kitabaki kuwa  mazingatio na kunikumbusha kuwa safari yetu ni mmoja.
Nikiwa bado namkumbuka Mwangamila rafiki yangu wa kubadilishana mawazo na mijadala mipana yenye tija ya kujifunza kila kukicha.Nilimkumbuka zaidi siku ya mahafali (2015) na nilimkumbuka zaidi Amina Sanani wote walinipa uzuni kwa kiwango tofauti,ilinipa wakati mgumu kujiona nipo katika sherehe yangu muhimu.Wote wawili hawa kuweza kuwepo kwenye mahafali kwa sababu tofauti nisingependa kuzijadili kwa upana au urefu wake lakini ni mipango ya Allah.
Siku zikapita baaada ya mahafali lakini Ilipofika Jumatano niliuliza Amina Sanani  anaendeleaje niliambiwa anaendelea vizuri na ametoka Dodoma yuko Bagamoyo nikaomba zitafutwe taarifa zaidi kuhusu hali yake  kisha nikasisitiza tuendele kumuombea mwezetu.
Lakini sikujua kuwa nyakati zinakalibia na hata kuwa pamoja nasi.Nakumbuka Ilipofika Alhamisi taarifa ikatolewa kuwa Amina hayupo tena nasi.Mwili ulinyongonyea na moyo uliumia lakini nikajisemea “Kwa Allah sote tutalejea’’.
Nilikumbuka siku ya kwanza kusungumza na Amina Sanani ilikuwa Makumba Bay,Moshi.Tulijadili mambo mengi lakini nakumbuka alikuwa msikivu na alipenda kupamanisha hoja ili kupata wazo bora zaidi.Hakuwa mtu wa kuangalia nani kasema ila aliangalia  umesema nini kwa msingi upi na uzito wake ni upi.Nakili kuwa ilikuwa siku nzuri sana kwa kuwa ubongo wangu ulipata mawazo mapya na kutoa mawazo mapya kuhusu maisha.

Nilipenda nijadili mambo mengi  muhimu leo lakini nitasema machache na mengine nitaeleza siku za usoni.Nakumbuka Amina alipenda sana kutumia nukuu hii ‘’Girls live by dreams’’ kisha nikajisemea amejitaidi sana kufikia ndoto zake kama kijana lakini leo ameondoka.Sisi tuliobaki lazima tujifunze kuwa na ndoto ili tukiondoka tuache mawazo ya ndoto zetu au tuache ndoto iliyotekelezeka kwa faida yetu na wengine.Amina alijua umuhimu wa ndoto na aliamua kushikilia kauli mbiu yake kwa dhati kabisa tuseme alimanisha ‘’Amina live by dreams”.
Nakumbuka 2012 nikiwa mwaka wa kwanza  tulikuwa na jukumu la kuwasilisha mada na kuhakikisha wanafunzi wenzetu wanapata hamasa ya kuchangia mjadala  na kuelewa mada hiyo kwa upana wake.Ilikuwa katika somo la ‘’Genera Studies’’ na somo hili lilijumuisha wanafunzi kutoka fakati mbalimbali na mawazo tofauti yalikutana kisha kupambana na kusuguana kwa kiwango cha juu zaidi.
Nakumbuka wanafunzi walikuwa wengi na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwasilisha mada mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu na nilijianda vizuri ili kuhakikisha naweka rekodi sawa na heshima kama mtaji wa siku za usoni.
Nakumbuka mimi nilikuwa mzungumzaji wa tatu na nilijitaidi kuwa na mifano mingi na maelezo mazuri.Baada ya mimi na wanafunzi wenzangu kumaliza uwasilishaji wa mada,wanafunzi wenzetu walitupongeza  kisha  Mhadiri  alihitimisha mjadala.
Nakumbuka jambo mmoja muhimu baada ya mnyukano ule wa mawazo alitokea mtu mmoja tuu aliyeniambia ‘’Congratution you did it Kiduo!’’ maneno haya machache yamenijenga sana na nilijifunza  tabia ya kuwapa wengine moyo wa kujituma zaidi na nimepata hamasa zaidi kila nikijianda kujadili mada na limenisaidia kupenda kujisomea zaidi ili katika mijadala niendele kuwa bora zaidi.Nitakumbuka sana mchango huu uliotukuka wa maneno mchache ya Amina Sanani.Tuseme lada Amina alielewa mapema uwezo wa kujadili utanijenga na kunisaidia siku za usoni.


Ilipofika mwaka 2015 nilipoamua kugombea Ubunge na kuwaeleza wanafunzi wenzangu na kumbuka  Amina alikuwa mtu wa kwanza kupenda kunitania Mhe.Mbunge, kwangu ilikuwa faraja kubwa kwa kupata hamasa yake ya kuonyesha kuwa mpango wa kugombea utafanikiwa.Nilipopitisha karatasi ya mchango Amina alikuwa mmoja wa watu walionichangi kwa maneno machache napenda niseme alitoa baraka zote na hamasa katika moyo wangu ya kuendelea kusonga mbele.
 Japo siku fanikiwa kuwa mgombea lakini niliweza kujenga msingi wa safari ya kuwa tumikia wananchi siku za usoni.Najua kwa uwezo wa Allah siku mmoja nitafanikisha lengo la kuwa tumikia wananchi.Japo Amina ametangulia lakini ameniacha na mchango mkubwa katika safari yangu ya kisiasa.
Jambo la mwisho ambalo nitalikumbuka sana,hadi namiliza chuo kuna watu watano ambao nimebadilishana nao sana mawazo na tumekuwa marafiki wakaribu sana lakini hadi sasa wawili wametangulia mbele za haki (Prof.Mwangamila na Amina Sanani) watu hawa kila mmoja alikuwa na sifa zake lakini kwa muda mfupi sana niliweza kujifunza mengi kutoka kwao na wao walijifunza mengi kutoka kwangu na naona ni jukumu langu kuangali  mawazo walio kuwa wanafanana na yale waliotofautiani kwa namna gani naweza kutekeleza ili ya saidie kizaizi cha leo na kijacho.


Prof.Mwangamila  na Amina Sanani pumzikeni kwa Amani.Bado nakumbuka mawazo yenu muhimu na dunia itajifunza mengi kutoka kwenu ikiwa nitafanikisha kuelimisha, kujadili, kutekeleza na kusimamia mawazo yenu.Allah akipenda nitatimiza na tutakuwa pamoja siku mmoja.
Pole kwa wazazi wa Amina Sanani,mtoto wake,familia,wanafunzi wenzake na watu wake wa karibu.Tujifunze mema yake na tujuwe kuwa safari yetu ni mmoja kama sio mimi kufuata basi wewe au yule.
Napenda ni hitimishe kwa kusema najivunia na kufurahi kujifunza kutoka kwa watu hawa wawili Prof.Mwangamila na Amina Sanani.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA