JIJI LA ARUSHA LAJIPANGA KUONDOA MAKAZI HOLELA
Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro (kushoto)akiweka saini makubaliano
kati ya Jiji la Arusha na kampuni ya Bondeni Seeds Limited
yatakayowezesha eneo la Heka 750 kupimwa na kuwa kwenye mpango
unaoendana mpango Mji wa Jiji katika eneo la Murieti wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita,Mbunge wa
Arusha Mjini,Goodbless Lema,Mwanasheria wa Jiji,Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Jiji,Juma Idd na Mwanasheria wa Bondeni Seeds Limited
leo.
Meya wa
Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akibadilishana hati za makubaliano
na Mkurugenzi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited ,Rakesh Vohora ya
kuendeleza eneo la Heka 750 eneo la Muriet linalomilikiwa na kampuni
hiyo.
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Juma Idd (kulia) akifafanua
umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo, kushoto ni Meya wa
Jiji la Arusha,Calist Lazaro.
Diwani wa
Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji
la Arusha, Metson Paul (kushoto) akiwa Mwanasheria na Mkurungezi wa
kampuni ya Bondeni Seeds Limited.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo.
Halmashauri
ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds
Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa
Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya Jiji.
Meya wa
Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano
hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo
yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato
yanayotokana naupimaji huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na
mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi
inavyotaka.
“Hatutaweza
kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na
mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini
na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.
Mbunge wa
Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa
kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi
holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya
maji kubomoa nyumba zao.
Imeandaliwa na RWEYEMAMUINFO
0 comments:
Post a Comment