SIMBA YATOA GUNDU LA MAPINDUZI KWA KUMCHAPA MTIBWA
Pamoja
na kufungwa, Mtibwa Sugar walionyesha upinzani kwa Simba SC na dakika
ya 11, kiungo Shiza Kichuya alipoteza nafasi ya wazi baada ya shuti lake
kuokolewa na kipa Vincent Angban, raia wa Ivory Coast.
Dakika ya 44, Ally Shomari naye alipiga shuti kali, lakini kipa wa Simba SC, Vincent Angban akaokoa.
Kizza naye alipoteza nafasi za kufunga dakika ya 15 na 33 baada ya kupiga nje.
Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamani, lakini matokeo hayakubadilika.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Danny Lyanga dk64, Hamisi Kiiza/Awadh Juma dk89 na Peter Mwalyanzi/Said Ndemla dk31.
Mtibwa Sugar; Said Mohamed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Salim Mbonde, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Hussein Javu/Jaffar Kibaya dk64, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Mohammed Ibrahim/Vincent Barnabas dk64.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Prisons imeifunga Toto 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United imeifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mbeya City imeifunga 1-0 Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na Majimaji Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mchezo kati ya vinara wa Ligi Kuu, Azam FC dhidi ya African Sports unafuatia sasa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, wakati kesho mabingwa watetezi, Yanga wataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara.
0 comments:
Post a Comment