Thursday 18 February 2016

MWINJILISTI AFUNGUKA::MANABII WA UONGO JITOKEZENI MUWAOMBE RADHI WATANZANIA

Daudi Mashimo
Mwinjilisti wa Kanisa la Calvary la huduma ya Injili la maumivu ya uponyaji  la Mwenge jijini Dar es Salaam Daudi Mashimo amewataka watumishi wanaojiita manabii kujitokeza kuomba msamaha kwa Watanzania  ndani ya siku 14 kwa kudanganya kuwa wao ni manabii.
Amesema kuwa kwa sasa Tanzania kuna mlipuko mkubwa wa Manabii wa uongo hivyo waache kujiita manabii na wajitokeze kuomba msamaha kwa Mungu na kwa taifa kwa ujumla kwani wote ni matapeli wa kiroho.
“Nabii ana sababu ya kuwepo na pia hana dini hivyo Mungu mwenyewe ndiye anaempa ujumbe kuja kutoa kwa wahusika na hao wanaojiita  manabii hawana sifa ya kuwa manabii bali ni wapigaji kwani huduma wanazozifanya si za kinabii” alisema Mashimo.
Ameongeza kuwa kwa sasa nchi yetu imegubikwa na mambo mengi sana hivyo kama nabii anapaswa kufahamu mambo hayo kwa ajili ya kusimama ili kuponya taifa kwa kutahadharisha katika mambo mbalimbali ambayo yanatarajia kutokea.
Daudi Mashimo
Mwinjilisti wa Kanisa la Calvary la Huduma ya Injili la maumivu ya uponyaji  la Mwenge jijini Dar es Salaam Daudi Mashimo akifafanua jambo toka katika  maandiko matakatifu kwa waandishi wa habari. (Picha zote na Ally Daudi MAELEZO)
“Nabii anajulikana kwa matendo yake hivyo wanaojiita manabii ni matapeli wa kiroho hakuna wa kweli hata mmoja hivyo  wanapaswa kutubu mbele za Mungu na kuacha mara moja kujiita kuwa wao ni manabii” alisema Mwinjilisti huyo.
Amewataja nabii ambao si wa kweli kuwa ni pamoja na  nabii Joe David wa Ngurumo ya upako la Arusha, Mkombo wa Boko Magengeni,  Mtume na Nabii kimbilio wa segerea,  Malisa wa  Mwanza, Milili wa  kinondoni Studio  na wengine wote wanojiita nabii na kusisitiza kuwa waache mara moja kujiita nabii.
Mbali na hayo watanzania wanapaswa kuwa makini na kuepukana na manabii wa uongo ili kukomboa taifa kwa ujumla.
Imeandaliwa na Nyakongo Manyama-Maelezo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA