Friday 15 April 2016

EUROPA:: LIVERPOOL YAUDUWAZA ULIMWENGU WA SOKA NA KUTINGA NUSU FAINALI

The Liverpool players acknowledge the support from the Kop with the victory and a place in the semi-final secured
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia mbele ya mashabiki wao baada ya mechi kumalizika
TIMU za Liverpool, Shakhtar Donetsk na Villarreal zimetinga Nusu Fainali ya michuano ya Europa League 2016 baada ya mechi za marudiano usiku wa Alhamisi. 
Reus and Aubameyang celebrate as the momentum fell back to Dortmund following a merciless finish from the German international 
Marco Reus pamoja na Aubameyang wakishangilia baada ya Reus kupachika bao la tatu 


Liverpool imesonga mbele baada ya kuifunga 4-3 Borussia Dortmund Uwanja wa Anfiled, hivyo kufuuz kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya wiki iliyopita kutoa sare ya 1-1 Ujerumani.

Striker Aubameyang celebrated his goal, which cemented Dortmund's advantage in the tie, with his trademark acrobatics
Mshambuliaji wa Dortmund Aubameyang akishangilia baada ya kupachika bao la pili kwa kuruka sarakasi 


Mabao ya Liverpool yamefungwa na Divock Origi dakika ya 48, Philippe Coutinho dakika ya 66, Mamadou Sakho dakika ya 77 na Dejan Lovren dakika ya 90 na ushei, wakati ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya tano, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya tisa na Marco Reus dakika ya 57.

Origi (right) gave Liverpool hope with a composed finish early in the second half, threading the ball under goalkeeper Roman Weidenfeller 
Mshambuliaji wa Liverpool Divok Origi akiifungia timu yake bao lakwanza katika dakika ya 48

 Katika mchezo huu ambao umewaduwaza wengi katika ulimwengu wa soka  Liverpool walikonekana kupotea kabisa baada ya kuruhusu mabao mawili katika dakika kumi za mwanzo lakini hatimaye kupata magoli manne katika kipindi cha pili na kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
Dejan Lovren akienda hewani kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya mwisho Uwanja wa Anfield 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA