Saturday 23 April 2016

MKUU WA WILAYA MOSHI AZINDUA RASMI SHINDANO LA MISS KILIMNAJARO 2016



Baadhi ya warembo ambao ni washiriki wa Miss Kilimanjaro 2016 wakifungua vinywaji aina ya "shampein" kuashiria uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu
Mmoja kati ya waaandaji wa hafla hiyo akimminia kinywaji Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga aina ya "shampein" iloyofunguliwa kama ishara ya kuwa shindano limefunguliwa rasmi
Jana,Mkoa wa Kilimanjaro kushuhudia hafla ya uzinduzi wa shindano la kumsaka mlimbwende atakayewakilisha mkoa huo katika ngazi ya Miss Tanzania uliohudhuriwa na mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na kuzinduliwa rasmi na  Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini Mh. Novatus Makunga .
Washiriki wa Miss Kilimanjaro 2016 wakionesha umahiri wao katika kucheza mbele ya wageni waliohudhuria halfa hiyo
Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na washiriki wa Miss Kilimanjaro 2016
Naye muandaaji wa shindano hilo katika mkoa wa Kilimanjaro Bi. Dotto Sang’wa mkurugenzi wa kampuni ya Dee's Bridal Entertainment  inayojihusisha na masuala ya kupamba maharusi aliweka wazi dhamira ya kulifanya katika ubora wa aina yake sanjali na kuhakikisha linakuwa mfano wa kuigwa huku akiitaja tarehe ya fainali kuwa ni tarehe 27 ya mwezi wa tano.
Muandaaji wa Miss Kilimanjaro 2016 Bi.Dotto Sang'wa akitoa utangulizi katika hafla hiyo

“Tumejipanga kuhakikisha tunabadili muono wa jamii katika tansia ya urembo kwa kuhakikisha kuwa warembo wetu( wanaoshiriki shindano kwa mkoa wa Kilimanjaro) wanapata mafunzo bora kabisa wakiwa kambini hasa tukilenga wakaitumikie jamii kwa dhati na kwa hili tunahitaji ushirikiano wenu sana” aliongeza Bi. Dotto.
Kutoka kushosho ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Moshi Mjini Afande Omary Ntungu ,Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi Ndg.Raymond Ngoya, Mkuu wa wilaya ya Moshi Mh. Novatus Makunga, mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga mara baada ya zoezi la uzinduzi 
Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Salonero nje kidogo ya mji wa Moshi ilihidhuriwa na mstahiki meya wa manispaa ya Moshi mjini Raymond Ngoya , Kamanda wa Polisi wilaya ya moshi Afande Omary Ntungu pamoja na wawakilishi wa kampuni mbalimbali.

Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini Mh. Novatus Makunga akitoa hotuba fupi kabla ya zoezi la uzinduzi wa shindano hilo
Akizungumza wakati anazindua,Mh Novatus Makunga alieleza kuwa sasa umefika wakati wa wanakilimanjaro kumuunga mkono muandaaji ili kuhakikisha Kilimanjaro kwa ujumla inafika mbali katika mashindano ya ulimbwende katika ngazi zote.

Mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga (kushoto) akimkabidhi katiba ya uendeshaji wa mashindano ya ulimbwende kwa muandaaji wa shindano hili katika mkoa wa Kilimanjaro Bi. Dotto San'gwa
Aidha wakati akielezea historia fupi ya mashindano ya ulimbwende kitaifa pamoja na kukabidhi katiba ya uendeshwaji wa miss Tanzania kwa muandaaji wa shindano hili mkoa wa Kilimanjaro, mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga alisema miongoni mwa jambo la kustaajabisha ni kwamba asilimia kubwa ya washindi wa miss Tanzania kitaifa wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro.
Muandaaji wa Miss Kilimnjaro 2016  Bi. Dotto Sang'wa akionesha katiba kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo
“Kweli hili suala ni la kufurahisha lakini ajabu ni kwamba hawa wanaoshinda wengi wao huwa wanawakilisha sehemu nyingine tofauti na Kilimanjaro ambapo ndipo kwao, sasa hii iwe changamoto kwenu wana Kilimanjaro hakikisheni mnawaunga mkono hawa mabinti wa nyumbani ili nao waone kuwa kutokea hapa hapa nyumbani inawezekana” alihitimisha .



Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA