Friday 13 May 2016

BAADA YA KUOKOKA, KAJALA AKEJELIWA

BAADA ya kukiri  kuwa ameamua kuokoka na kumrudia Mungu, mrembo kunako filamu za Kibongo, Kajala Masanja amekejeliwa na baadhi ya watu wake wa karibu.
KAJALA623
Akizungumza na Amani Kajala alisema kitendo cha kuokoka kimegeuka kama kejeli kwa marafiki zake ambapo wengi humcheka lakini anaamini kabisa siyo akili zao bali shetani anataka kuwatumia ili aanguke.
“Kuna ambao wananicheka kicheko kikubwa kabisa baada ya kusikia kuwa nimeamua kumfuata Yesu na wengine kunikejeli lakini mimi sina neno naamini kabisa ni nguvu ya shetani ili nirudi nilikotoka, nawaambia tu watakuwa wamechelewa sana,” alisema Kajala.

Chanzo: GPL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA