MABAKI YA NDEGE YA EGYPTAIR YAONEKANA UGIRIKI
Mabaki ya ndege ya EgyptAir MS804 iliyoanguka yameonekana kusini mwa kisiwa cha Ugiriki cha Karpathos, Shirika la Anga la Misri limethibitisha.Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ilikuwa ikitokea Jijini Paris kwenda Cairo ikiwa na abiria 66 na wahudumu wakati ikianguka.
Wizara ya usafirishaji jijini misri zimethibirisha
kupatikana kwa mabaki ya ndege iliyokuwa
imepotea iliyokuwa ikitoka kairo kuelekea misri MS 804 karibu na kisiwa cha
Karpathos ripoti za kiwanja haicho kilithibisha kupatikana na mabaki ya ndege
hiyo hivyo basi kampuni hiyo imetoa salamu za rambirambi kwa familia ya watu
waliokuwepo na wahudumu wa ndege hiyo.
Kwa sasa kundi la
wachunguzi wa Misri wakishirikiana na wenzao wa Ugiriki wanaendelea kutafuta
mabaki mengine ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa
imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa
Ufaransa. Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia
mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria,
Sudan, Chad na Ureno.Awalia rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema
kuwa ndege hiyo ilianguka.
Makamu wa rais wa Misri Ahmed Adel ameliambia shirika la habari la CNN operesheni ya uokoaji imeanza kufanya jitihada za kuyafikia mabaki ya ndege hiyo.
0 comments:
Post a Comment