PICHA::MASHABIKI WA SEVILLA NA LIVERPOOL WALIVYOTWANGANA WAKATI WA FAINALI YA EUROPA LIGI
Mchezo wa fainali wa ligi ya Europa uliozikutanisha timu za Sevilla toka Hispania na Liverpool toka Uingereza na kumalizika kwa Sevilla kulitwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo, ulishuhudia vurugu toka kwa mashabiki wa timu zote mbili. Mchezo huo uliofanyika Basle katika uwanja wa St Jakob-Park, ulimalizika kwa Liverpool kuchapwa 3-1
Vurugu hizo zilitokea katika moja ya jukwaa ambalo lilitumiwa na mashabiki wa timu zote mbili ambapo ngumi na mateke zilitawala huku mashabiki wa Sevilla wakionekana kuwa chanzo na wenye fujo zaidi.

0 comments:
Post a Comment