Tuesday, 31 May 2016

MSAKO: FAHAMU ZAIDI KUHUSU HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO


MSAKO ni kipengele maalum katika Blog hii ambacho kimelenga kutafuta na kukuletea makala fupi zenye dodoso muhimu juu ya masuala mbali mbali duniani ikiwemo mazingira,utalii, siasa, michezo na maendeleo.
Katika makala yetu leo tumekuletea dodoso kuhusu Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Hifadhi  ya mlima  Kilimanjaro ilianzishwa  rasmi  mnamo  mwaka 1973 na  ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.

Ukweli halisi  wa mambo  jina “Kilimanjaro” kutokana na maelezo ya wenyeji asilia  wachaga wa Mkoa huu waishio maeneo haya ya mlima ni kwamba neno “Kilimanjaro”limetokana na neno   la Kabila  la Wachaga “Kilema Kyaro” likimaanisha  safari  iliyoshindikana au isiyowezekana . “Kilema’ inamaanisha  kisichowezekana  au  kilichoshindikana na neno “Kyaro” likimaanisha safari. Tafsiri rahisi hapa  ina  maana ya  kwamba  safari  ya matembezi kuelekea kupanda kilele cha mlima kilikuwa  kikiwashinda watu wengi waliojaribu  kupanda mlima na hii ilikuwa  wakati wa kipindi  cha nyakati  hizo za miaka ya zamani.  Leo hii hali  hiyo  haipo tena kwa sababu  wengi  wa watalii  kutoka  nje ya  nchi  na ndani  ya nchi  hufika  kileleni  mwa  mlima  pasipo shida yeyote  ile. Hifadhi  hii kama inavyojieleza,  kijiografia  inapatikana mkoani  Kilimanjaro.



kileleni
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia. 
Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.

Hifadhi hii inafikika kwa njia ya barabara  umbali  wa kilomita 48 kutoka  mji  wa Moshi  ambao  ndio  makao  makuu ya mkoa  wa Kilimanjaro. Vile vile hifadhi hii  inafikika umbali wa kilomita 128 kutoka  mkoani  Arusha. Inachukua  mwendo  wa dakika  50 kutoka  Moshi  Mjini, vile vile  ni  mwendo  wa saa 1 kutoka  kiwanja  cha ndege  cha  kimataifa cha  Kilimanjaro (KIA). Hali kadhalika ni saa 2.30 kutoka  mkoani  Arusha. 
Spencer West, raia wa nchini Canada, 31, asiye na miguu ameukwea mlima mrefu kuliko yote barani Afrika, Mt. Kilimanjaro kwa kutumia mikono
Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni, na njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi.
Wanyama kadhaa hupatikana katika msitu unaozunguka Mlima Kilimanjaro wakiwemo mbega, nyani, nyati, chui, tembo, swala na ndege.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA