Monday, 20 January 2025

WAZIRI JAFFO AIPONGEZA TCAA KWA UFANISI SEKTA YA USAFIRI WA ANGA




Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo, akiwa katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)





Timu  ya maonesho ya TCAA ikiendelea kuwahudumia na kutoa elimu kuhusu fursa mbalimbali katika sekta ya usafiri wa anga.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo, alitembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Akiwa hapo, aliipongeza TCAA kwa usimamizi thabiti wa sekta ya usafiri wa anga na alipata maelezo kuhusu utendaji wa Mamlaka pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Maonesho haya yaenga kuonyesha mafanikio ya Zanzibar katika sekta mbalimbali tangu Mapinduzi ya mwaka 1964, na yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wananchi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA