Monday 2 May 2016

RAIS KABILA AUNGANA NA MAELFU YA WATU NCHINI DRC WALIOJITOKEZA KUUAGA MWILI WA PAPA WEMBA


Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamejitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mwanamuziki nyota Papa Wemba katika siku ya kwanza ya zoezi hilo.

Mwili wa Papa Wemba umewekwa kwenye jengo la bunge Jijini Kinshasa na baadaye utapelekwa nyumbani kwa familia yake kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho.

Papa Wemba aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66, baada ya kuanguka jukwaani nchini Ivory Coast Aprili 24, atazikwa siku ya jumatano.
                   Jeneza lenye Mwili wa Papa Wemba likiwa ndani ya jengo la Bunge
                                            Marehemu Papa Wemba akiimba enzi za uhai wake

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA