Tuesday 3 May 2016

CHELSEA WAMEKABIDHI::::LEICESTER CITY BINGWA EPL 2015/2016




Hakuna utata sasa ila ni kusema kuwa Leicester City ndiyo mabingwa wapya wa England msimu huu 2015/2016.

Leicester City wanapokea kombe hilo kutoka kwa Chelsea ambao msimu huu, wamechemsha.

Lakini Chelsea, ndiyo waliowapa Leicester ubingwa huo baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham waliokuwa wakiuwania kwa nguvu zote na sasa Leicester City watakabidhiwa Kombe hilo katika uwanja wao wa nyumbani watakapowakaribisha Everton wikiendi hii.

Leicester stars celebrate winning the title at Jamie Vardy's house after watching Chelsea
Pichani anaonekana mshambuliaji mahiri wa Leicester City Jamie Vardy (ktikati) akisherekea ubingwa akiwa na wachezaji wenzake
 Chelsea ambao walikuwa wameshakubali mabao mawili kufikia mapumziko walirejea na kujivua ubingwa rasmi na ni Eden Harzad aliyekabidhi ubingwa huo baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika ya 83 ya mchezo.


Sare hiyo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, unaifanya Spurs kubaki na pointi 70 huku Leicester wakiwa na 77 ambazo hakuna timu inayoweza kuzifikia.
Young Leicester fans celebrate outside Vardy's house after they are confirmed as Premier League winners
Mashabiki wa Leicester wakiwa mitaani kusherekea ubingwa
Miongoni mwa jambo lenye hisia katika msimu huu ni namna Leicester City walivyoduwaza ulimwengu wa soka kwa kuvipiku vilabu vigogo na kutangaza ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia.
Thai Buddhist monk Phra Prommangkalachan holding a banner emblazoned with sacred patterns surrounding Leicester City Football Club's crest as he poses for pictures at the Traimitr Withayaram Woraviharn Temple in Bangkok

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA