Sunday, 29 May 2016

SAMATTA AIPELEKA GENK EUROPA LEAGUE



Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).
Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.

Katika ushindi huo wa magoli 5-1, Samatta amefunga goli moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo. Nikolaos Karelis ambaye amfunga hat-trick kwenye mchezo huo alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 17 kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45 na kuipeleka Genk mapumziko ikiwa mele kwa magoli 3-1.
Kipindi cha pili Karelis aliongeza bao la nne dakika ya 56 kisha kukamilisha hat-trick yake dakika ya 71 kwa kufunga bao la tano.

Mchezo huo ulikuwa ni wa marudiano, mchezo wa awali Genk walipoteza kwa bao 2-0 kwa maana hiyo hiyo Genk wamefuzu kucheza michuano ya Europa ligi kwa matokeo ya jumla 5-3.
Genk itaanzia kwenye hatua ya awali ya mtoano kabla ya ile ya makundi, kama watafuzu basi watapangwa kwenye hatua ya makundi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA