Sunday 29 May 2016

USIPITWE NA TAKWIMU HIZI MUHIMU KUHUSU FAINALI YA UEFA 2016

Real Madrid wametwaa taji la ubingwa wa vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya 11 baada ya kuichapa Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati kwenye uwanja wa San Siro mjini Milan. Bao la Sergio Ramos liliwaweka mbele vijana wa Zinedine Zidane kabla ya striker wa Atletico Antoine Griezmann hajakosa penati.
Mabadiliko yaliyofanywa na Diego Simeone kumuingiza Yannick Carrasco yaliupeleka mchezo huo extra time baada ya kuisawazishia timu yake kipindi cha pili. Cristiano Ronaldo alipachika wavuni penati ya ushindi baada ya Juanfran kukosa penati yake kwa upande wa Atletico.

Hebu angalia takwimu hizi muhimu
  • Atletico sasa imekuwa ni klabu iliyofika mara nyingi (mara tatu) kwenye fainali ya European Cup/Champions League na kushindwa kutwaa taji hilo
  • Hii ilikuwa ni fainali ya nane ya Champions League kufika hadi extra-time, nay a saba kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.
  • Zinedine Zidane ni kocha wa pili (baada ya Miguel Munoz) kushinda la European Cup/Champions League akiwa kama mchezaji na baadaye kocha wa Real Madrid.
  • Zinedine Zidane ni kocha wa kwanza kutoka Ufaransa kushinda Champions League.
  • Sergio Ramos amekuwa mchezaji wa tano kufunga kwenye michezo miwili tofauti ya fainali ya Champions League huku akiwa beki wa kwanza kufanya hivyo (Raul, Samuel Eto’o, Lionel Messi and Cristiano Ronaldo).
  • Ramos ameungana na Messi pamoja na Eto’o akiwa miongoni mwa wachezaji watatu kufunga magoli kwenye fainali zao mbili za kwanza za Champions League.
  • Antoine Griezmann amekuwa mchezaji wa kwanza kukosa penati  kabla ya zile za kutafuta mshindi kwa changamoto ya matuta. Mara ya mwisho Arjen Robben alifanya hivyo mwaka 2012 dhidi ya Chelsea.
  • Marcello Lippi ndiye kocha aliyepoteza fainali nyingi za Champions League (tatu)  akifatiwa na Diego  Simeone (mbili).

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA