Saturday 30 July 2016

MKUU WA WILAYA IRINGA, MH KASESELA ASHIRIKI UZINDUZI WA KANISA LA EFATHA MLIMA WA SAYUNI MTAA WA LUGALO B WILOLESI

Nabii Mwingira wa Kanisa la Efatha akizindua rasmi Kanisa la Efatha Mlima wa Sayuni katika mtaa wa Lugalo B Wilolesi Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo ameshiriki uzinduzi wa Kanisa la Efatha Mlima wa Sayuni katika mtaa wa Lugalo B Wilolesi Iringa. 

Akitoa salamu za serikali, alisema maarifa huyapati kwa kuomba tu bali ni ile hali yako ya uelewa na ukafanya unavyo elewa huku ukimtegemea Mungu. 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiongea katika uzinduzi wa Kanisa la Efatha Mlima wa Sayuni katika mtaa wa Lugalo B Wilolesi Iringa.

Akaendelea " tunapokataa kukaa na Mungu Mungu naye hutuacha nasi tutaendelea kutumia akili zetu, akili zetu bila Mungu ni kazi bure" Mh Kasesela alimuomba Mtumishi wa Mungu Josephat Mwingira kuuombea mkoa wa Iringa uondokane na dhambi zinazotutenganisha na Mungu ikiwemo ubakaji, ushirikina na kutenda haki kwa kila mtu.

Naye Nabii Mwingira akifungua ibada alisema sasa Tanzania ipo katika mabadiliko y majira ya Mungu, elimu iliyopo itabadilika iendane na mfumo wa Mungu, ni lazima Taifa liondokane na elimu ya kitumwa ambapo kila amalizae shule anatafuta kuomba kazi ili awe mtumwa wa mwingine, aliendelea " Ukimuona mtu amemaliza shule anahangaika mitaaani na barua za kuomba kazi ujue huyo hajaelimika bali kaenda shule" 

Nabii Mwingira anaendelea na maombi na mahubiri kesho katika milima ya Sayuni pale wilolesi kuaanzia saa 3 asubuhi Kabla ya kuelekea Mbeya jumapili.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela lakipongezana na Nabii Mwingira mara baada ya uzinduzi wa Kanisa la Efatha Mlima wa Sayuni katika mtaa wa Lugalo B Wilolesi Iringa.
                                                                                                                       Ni furaha 

Nabii Josephat Mwingira  akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela mara baada ya uzinduzi

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA