Friday 22 July 2016

TANZIA:: COMEDIAN KUNDAMBANDA AFARIKI DUNIA

Taarifa za awali zinaeleza kuwa msanii  wa vichekesho Ismail Issa Makombe maarufu zaidi kama KUNDANBANDA amefariki dunia nyumbani kwao Masasi mkoani Mtwara huku.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu Kundambanda amefariki alfajiri ya leo mjini Masasi.Alikuwa shambani kwake takribani mwezi mmoja uliopita akiendelea na shughuli za kilimo cha ufuta, wiki iliyopita alirudi Masasi kuendelea na shughuli zake zingine, ndipo majuzi alibanwa na kifua akaenda mwenyewe hospitali huku akiendesha gari yeye mwenyewe akapatiwa matibabu na jana kuanzia mchana ndipo hali ilipobadilika na hatimaye leo alfajiri kufariki dunia.
 
Kundambanda alijipatia umaarufu kupitia kundi la vituko show ambapo zaidi alikuwa akiigiza kama askari wa kitengo cha barabarani "Trafiki" na kutumia lafudhi ya watu wa Mtwara. Sambamba na hilo Kundambanda katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka jana alikuwa gumzo hasa pale alipojitokeza na kuwa  mgombea ubunge jimbo la Masasi kupitia tiketi ya CUF  na kuleta hali ya sintofahamu ndani ya UKAWA hasa ambapo  Dr. Makaidi aliesimamishwa kupitia NLD ndiye aliyekuwa mgombea rasmi kupitia umoja huo kabla mauti hayajamkuta zikiwa zimebakia siku chache kufikia kilele cha kampeni.
Lakini hata hivyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD) Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM.
Kundambanda akiwa jukwaani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015
Kifo cha Kundambanda kimekuwa pigo jingine kwa kundi la VITUKO SHOW hasa likiwa limempoteza aliyekuwa mchekeshaji wa kipekee Mohammed Abdallah  maarufu "KINYAMBE".

Tayari baadhi ya wasanii wameonesha kuguswa na msiba huu na kuanza kuweka post katika mitandao ya kijamii.




Nimekuwekea moja kati ya kazi alizofanya katika kundi la vituko Show

 Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea FUNGUKA LIVE.COM

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA