Thursday 28 July 2016

WAZIRI MKUU AKABIDHIWA MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA DAR


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo kukbidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salaam Julai 28, 2016.Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Temeke baada ya kuwasili kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi kukabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Oisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait nchini, Jaseen Al Najem na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msigi ya Chamazi wakiwa wamekaa kwenye madawati mawili kati ya 300 yaliyotolewa na Kuwait ili kukabiliana na tatizo la madawati jijini Dar es salaa.
 Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. Waliosimama watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, , Augustine Mahiga, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Susan Kolimba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , Balozi Augustine Mahiga (kulia kwake) wakifurahi wakati , Bwana Murtaza Adamjee alipoongoza wimbo katika hafla ya kukabidhi madawati kwa mkoa wa Dar es salaam iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya wanafunzi na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati na fedha shilingi milioni 1000 kwa Waziri Mkuu kwenye shule ya Msingi yaChamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mlkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi, Augustine Mahiga (katikati) na Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora Nchini katika hafla ya kakabidhi madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa shule za Dar es salaam iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kupokea madawati na fedha shilingi milioni 1000 kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam Julai 28, 2016.Madawati ayo yalitolewa na Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ikishirikiana na Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA