EUROPA:::ADRUIZ ATUPIA 5 ,ATHLETIC BILBAO IKIIADHIBU GENK 5-3
MSHAMBULIAJI mkongwe raia wa Hispania anayekipiga Athletic Bilbao Aritz Aduriz amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye michuano ya Europa miamba hiyo ikiiua KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta mabao 5-3.
Aduriz mwenye miaka 35 alifunga hat-trick kwa penalti na kuwa Mhispania wa kwanza kufunga mabao matano kwenye michuano ya Ulaya tangu mwaka 1971.
Kwenye mchezo uliopita Genk waliwachapa Bilbao mabao 2-0 kwenye ardhi yake ya nyumbani huku Samatta akiingia kutokea benchi baada ya kutoka kwenye majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Mabao ya Genk yalifungwa na Leon Bailey, Onyinye Ndidi pamoja na Tino-Sven Susic.
Matokeo mengine ya mechi za Europa
FC Astana 1-1 Olympiacos
Anderlecht 6-1 Mainz 05
Sasuolo 2-2 Rapid Wien
Fenerbache 2-1 Man United
FC Astra 1-1 Victoria Plzen
FC Zenit 2-1 Dundalk
Zorya 1-1 Feyernood
Austria Wien 2-4 As Roma
FK Qabala 1-2 Saint Etienne
0 comments:
Post a Comment