Saturday 14 January 2017

KISA CHA KUSISIMUA::MTOTO ALIYEIBWA MAREKANI APATIKANA BAADA YA MIAKA 18


Mtoto wa kike aliyeibiwa mara tu baada ya kuzaliwa kwenye hospitali huko Jacksonville, Florida, Marekani amekutwa na polisi akiwa hai South Carolina baada ya miaka zaidi ya 18 kupita.

Kamiyah Mobley, ambaye aliibiwa Julai 1998, amepatikana baada ya kutolewa taarifa kwa mamlaka ya Walterboro, South Carolina, na kumfungulia mashtaka mwanamke mmoja Gloria Williams, 51, ya utekaji.

Msichana Mobley alikuwa akiishi kwa kutumia jina lingine la Alexis Manigo na akiamini mtekaji wake Bi. Williams ni mama yake mzazi. Wazazi wake wa kumzaa wametaarifiwa kupatikana kwa binti yao huyo.
                       Kamiyah Mobley akiwa na mama aliyemteka akiwa mchanga Gloria Williams
Mama mzazi wa Kamiyah Mobley akiangua kilio siku chache baada ya mtoto wake mchanga kuibiwa 1998
Baba mzazi wa Kamiyah Mobley, akishangaa kupata taarifa hizo ambapo alibainisha kuwa aliwahi kuongea uso kwa uso na mtoto huyo bila ya kujua kuwa ni mwanaye

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA