Saturday, 14 January 2017

MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE MAHAFALI YA 19 CHUO CHA DIPLOMASIA KURASINI

Ijumaa ya tarehe 13/01/2017 Chuo cha Diplomasia kilifanya mahafali ya 19 kwa ajili ya  kuwaaga na kutunuku vyeti kwa wahitimu zaidi ya 180 kwa ngazi  za Astashahada, Stashahada na Stashahada ya Uzamili yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha protokali kikiwa katika mipango ya kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa
Askari wa Bendi ya muziki ya Polisi wakiwaongoza wahitimu, meza kuu pamoja na wahadhiri Chuo cha Diplomasia kuingia katika ukumbi wa sherehe za mahafali ya 19 ya chuo hicho
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Diplomasia, Balozi Ombeni Sefue akiambatana na jopo la viongozi wa meza kuu kuingia katika ukumbi wa sherehe za mahafali ya 19 ya chuo hicho 


Meza kuu pamoja na Mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini wakiwa wima wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa


Baadhi ya Wahitimu katika ngazi ya Stashahada ya Uzamili wakitunukiwa hadhi ya elimu yao katika mahafali ya 19 ya chuo hicho


Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini wakiwa na nyuso za tabasamu wakati wa mahafali hayo
Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Benedict Theresia Msuya  ambaye alikuwa mwanafunzi bora katika ngazi ya stashahada ya uzamili  kozi Menejimenti ya Mahusiano ya Kimataifa akijongea kunako meza kuu kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi


Mgeni rasmi akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Benedict Theresia Msuya  ambaye alikuwa mwanafunzi bora katika ngazi ya stashahada ya uzamili  kozi Menejimenti ya Mahusiano ya Kimataifa.  


Mgeni rasmi akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wanafunzi bora katika ngazi ya Stashahada ya uzamili kozi ya Diplomasia ya Uchumi 


Askari wa Bendi ya muziki ya Polisi wakifurahia jambo katika mahafali hayo
Mwanafunzi  Chuo cha Diplomasia akitumia kipaji chake kutoa burudani kwa njia ya vichekesho katika mahafali hayo
baadhi ya wahadhiri wa Chuo cha Diplomasia wakifuatilia burudani katika mahafali hayo
Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wana-Protokali waliosimamia vyema taratibu nzima katika mahafali hayo

Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahadhiri wa Chuo cha Diplomasia
  

Sehemu ya wageni waliohudhuria mahafali hayo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA