Monday, 27 March 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AUBARIKI WIMBO WA NAY WA MITEGO, ATAKA AACHIWE HURU NA WIMBO WAKE UENDELEE KUCHEZWA REDIONI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo wa ‘WAPO’ na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Image result for nay wa mitegoAkiongea na Wandishi wa Habari Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa Kodi, wauza Unga, wanaotumia dawa za kulevya pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA