MHANDISI METHEW MTIGUMWE AWASHUKURU WADAU WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA –NANE NANE MWAKA 2017
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe
anawashukuru wananchi, wadau wa kilimo na Taasisi mbalimbali kwa kushiriki
Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima – Nane Nane mwaka 2017, ambapo
maadhimisho kwa ngazi ya Ki-Taifa yalifanyika katika Uwanja wa Maonyesho ya
Kilimo wa Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Aidha,
maadhimisho ya Ki-Kanda yalifanyika katika viwanja vya maonyesho ya John
Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni -
Dodoma; na Nyahongolo – Mwanza.
Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mhandisi
Mtigumwe amesema kuwa Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa
changamoto na kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira
hususani kwa vijana kwa kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.
Mtigumwe alisema kuwa Wizara,
taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo
wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji
kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.
''Ni matumaini yangu kuwa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi imetolewa ipasavyo lakini pia wadau walijionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi''
''Katika Maonesho hayo Teknolojia/Bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ikiwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo pia Taasisi za kitafiti zilionyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa'' Alisema Mtigumwe

Teknolojia na Bidhaa zingine
zilizoonyeshwa ni pamoja na uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa
teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni
ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zilionyesha ubunifu wa kumsaidia
mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo,
Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
Sikukuu ya wakulima inayofahamika
kuwa Nanenane husherekewa nchini kote kuanzia 1 Agosti mpaka tarehe 8 Agosti
kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika
na kilimo.
0 comments:
Post a Comment