Thursday, 28 September 2017

UONGOZI MPYA WA TFF WATEMBELEA SBL




Rais wa TFF ,Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani
alipofanya ziara katika Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.pembeni yake kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na kulia ni Mkurungezi wa masoko wa SBL Ceaser Mloka na mwishoni ni Kocha mkuu wa Taifa stars Salum Manyanga,Mapema jana katika ofisi za makao makuu ya SBL Temeke Jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie akifurahia jambo na Rais wa TFF ,Wallace Karia na Mkurungezi wa masoko wa SBL Ceaser Mloka wakati uongozi wa TFF ulipotembelea kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.



Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie akimkabidhi zawadi Rais wa TFF ,Wallace Karia mapema jana alipotembelea kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars katika ofisi za kampuni hiyo Temeke Jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam, Septemba 27, 2017. Uongozi mpya wa Shirikisho la Soko Tanzania (TFF) ukiongozwa na Rais wake Wallace Karia, leo umetembelea Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.  

Ziara hii imefanywa na uongozi mpya wa TFF ikiwa ni wiki moja kabla ya mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayozikutanisha Taifa Stars na Malawi, mchezo utakaofanyika  kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Tangu imepata udhamini wa SBL mwezi Mei mwaka huu, Taifa Stars imecheza mechi nne za kimataifa na kufanikiwa kuweka rekodi nzuri kwenye mechi zote ilizocheza.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Rais wa mpya wa TFF aliishukuru SBL kwa udhamini wake kwa timu ya taifa na aliihakikishia SBL kuwa uongozi wake umeunda  menejimenti ya Taifa Stars ili kuhakikisha kuwa timu ya taifa inapata ushindi kwenye kila mechi.

“Tunaishukuru SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika sana na ambao umeiwezesha timu yetu ya taifa kujiandaa vyema na mechi na kufanya vizuri kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa,” alisema Karia

Karia alisisitiza kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya udhamini wa timu ya taifa, zitatumika vizuri na kuongeza kuwa uongozi wa TFF unalenga kuongeza imani kwa wadhamini wa Taifa Stars na wadau wa soka kwa ujumla wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie alimpongeza Rais mpya wa TFF pamoja na timu yake kwa kuchaguliwa na kueleza kuwa SBL itaendelea kutoa misaada inayolenga kuendeleza michezo hapa nchini.
“SBL inatambua mchango muhimu ambao michezo inatoa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ndiyo maana tunaamini kuwa tunapoidhamini Taifa Stars, tunachangia katika kuwaburudisha na kuwaunganisha Watanzania wakiwa na bia yao bora ya Serengeti ikwa na ujumbe wake wa sifa yetu, bia yetu, nchi yetu,” alisema

Mwezi Mei mwaka huu, TFF iliingia mkataba wa ufadhili kwa Taifa Stars utakaodumu kwa kipindi cha miaka 3 utagharimu shilingi blioni 2.1na kuifanya SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa.

Ikizalishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996, bia ya Serengeti imetengenezwa na kimea kwa asilimia 100 huku ikiweza kushinda tuzo zaidi ya 10 kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa kutokana na ubora wake wa kimataifa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA