VODACOM YAJA KIVINGINE,YAZINDUA PINDUA PINDUA UNITS
Mtandao wa simu wa Vodacom umezindua huduma mpya kabisa ya matumizi iitwayo PINDUA
PINDUA UNITS ambapo imesheheni ofa
lukuki ikiwemo Whatsapp na Facebook bure huku upekee wake ni namna mtumiaji anapoweza kubadili matumizi ya units kulingana na uhitaji wake kwa wakati huo.
Akizungumza wakati wa kuzindua
huduma hii, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Bidhaa Vodacom Bi. Nandi Mwiyombella amesema
PINDUA
PINDUA UNITS imekuja kuleta mapinduzi ya huduma kwa watumiaji wa huduma za
kimawasiliano kwani inampa mteja uhuru wa kutumia dakika na Mb kivyovyote.
Naye Mkurugenzi wa Vodacom Bw. Ian Ferrao alipongeza jitihada hizi na kusema hili ni miongoni mwa huduma ya ubunifu zaidi na ya kipekee kuwepo hapa nchini huku akitoa rai kwa vijana pamoja na watumiaji wa mtandao kuchangamkia fursa hii adimu kufanya mawasiliano yanayowezesha mabadiliko kadiri ya uhitaji.
Jinsi ya kujiunga na Pindua
Pindua Units ni Kubonyeza *149*01# kisha kuchagua namba sita ambapo ni
Kifurushi cha PINDUA PINDUA UNITS na kuwa huru kujiunga na units za ujazo
wako ikiwa ni siku,wiki au mwezi.
"Nawasihi watumiaji wa Vodacom
kuitumia fursa hii adimu kabisa na vile vile niwashauri wasiotumia mtandao wetu
wajiunge ili waonje ladha kamili ya matumizi ya dakika pamoja na MB
inayopatikana katika PINDUA PINDUA UNITS." alihitimisha Bi Nandi Mwiyombella.
Kwa Maelezo Kuhusu Pindua Pindua Angalia Video Hii.
Mkurugenzi wa Vodacom Bw. Ian Ferrao akifuatilia jambo wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Pindua Pindua Units Mbele Ya Wafanyakazi Wa Vodacom Katika Ofisi Za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam |
Baadhi ya wafanyakazi pamoja na wadau waliohudhuria shughuli ya uzinduzi wa huduma ya Pindua Pindua Units katika ofisi za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam |
TUMEWEZAAAAAAA!!!!!!!! Wafanyakazi wa Vodacom wakifurahia mafanikio ya huduma hii ya kipekee ya Pindua Pindua |
Wafanyakazi wa Vodacom wakijfurahia huduma ya Pindua Pindua Units wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es salaam |
0 comments:
Post a Comment