WAKURUGENZI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KUNUA CHAKI ZINAZOZALISHWA MKOANI HUMO
1 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya
kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober
Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akikagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha
Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati
wa ziara ya kikazi
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye
ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimkabidhi boksi tano
za chaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya
kutembelea na kukagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki
cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati
wa ziara ya kikazi
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akisalimiana na Meneja wa kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color Ndg
Mukhtar Mahamood mara baada ya kuwasili kiwandani hapo
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akikagua mizinga ya nyuki mara baada ya kutembele kiwanda Uzalishaji
chaki, Mafuta ya Alizeti na Asali cha Fahari Kilichopo katika eneo la
Tambukareli Halmashauri ya Mji wa Itigi wakati wa ziara ya kikazi, Kulia kwake
ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu
Ukaguzi
wa kiwanda cha uzalishaji Chaki
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akikagua eneo la kutunzia Unga wa Gypusm katika kiwanda cha uzalishaji
Gypsum cha Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akizungumza
kwa njia ya simu na mmiliki wa kiwanda cha uzalishaji unga wa Gypsum cha
Sanjaranda Bw Rashid Said Rashid akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia
Mkuu wa Mkoa kuwa mpaka kufikia Januari 2018 uzalishaji wa Gypsum utaanza katika
eneo la Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi ili kurahisisha huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akiwa
kwenye shamba la Mkulima Juma Patrick na kujionea mikorosho inavyoharibika kwa
kukosa dawa ambapo alizungumza kwa njia ya simu na muwakilishi wa Bodi ya
Korosho akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa dawa za
kuua wadudu kwenye Mikorosho zitawasili kati ya Jumanne Septemba 26 na Jumatano 27, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi
akionyesha chaki bora zinazozalishwa Wilayani Manyoni Mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi
akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe Ally Minja mara baada ya
kuwasili Kwa ajili ya kutembelea Kiwanda vya usagaji unga wa Gypsum na
uzalishaji chaki.
Miongoni wafanyakazi wa kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color wakiendelea
na kazi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi
1 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema
Nchimbi akikagua kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color Halmashauri ya
Itigi
Na Mathias Canal,
Singida
Wakurugenzi wa
Halmashauri za Wilaya na Manispaa Mkoani Singida wametakiwa kuanzia Septemba
25, 2017 kuanza kununua chaki zinazozalishwa katika viwanda mbalimbali
vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Itigi Mkoani humo.
Pia Taasisi ya kuzuia
na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeagizwa kufuatilia Halmashauri
zitakazoendelea na hatua za manunuzi ya chaki nje ya Mkoa wa Singida ili ziweze
kuchukuliwa hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo.
Agizo hilo limetolewa
na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya ziara ya kikazi
ya kutembelea kiwanda cha uzalishaji Gypsum cha Sanjaranda, Kiwanda cha usagaji
wa unga wa Gypsum/Uzalishaji chaki cha Dober Color na Kiwanda cha uzalishaji
chaki cha Fahari.
Mhe Nchimbi alisema
kuwa ni aibu kwa Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla kuagiza chaki nje ya nchi
ilihali mkoani Singida zinazalishwa chaki zenye ubora, zisizo na vumbi la
kuwasumbua walimu na wanafunzi kuliko za nje ya nchi tena kwa kutumia malighafi
za ndani ya nchi.
Alisema Wakuu wa Wilaya
wanapaswa kusimamia zoezi hilo ili kutumia bidhaa bora zinazozalishwa ndani ya
Mkoa kwani zitaongeza ufanisi wa ajira kwa wananchi na kuwa na uwezo wa
kutengeneza soko la ndani ya Wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Alisema hakutakuwa na
maana yoyote katika Mkoa kama viwanda vinazalisha chaki lakini watumiaji wa
chaki hawanunui bidhaa hizo badala yake wananunua katika maeneo mengine.
Mhe Nchimbi aliwasihi
viongozi mbalimbali katika Wilaya na Mikoa mingine nchini kununua chaki
zinazozalishwa mkoani Singida huku akitoa unafuu kwa mikoa jirani na Mkoa wa
Singida ambayo ni Dodoma, Manyara na Tabora kutumia gharama za manunuzi pekee
huku serikali ikisimamia gharama zote za usafirishaji kuwafikia wanunuzi katika
mikoa yao.
Sambamba na hayo pia
Mhe Nchimbi aliziagiza Halmashauri zote mkoani humo kutangaza katika vyombo vya
habari bidhaa zilizopo ili kuwarahisishia watanzania kufahamu uzalishaji
unaofanywa na Mkoa wa Singida kwani kwa kufanya hivyo wafanyabiashara na
wawekezaji watatambua fursa zilizopo na kununua bidhaa mbalimbali jambo ambalo
litakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.
Aliwapongeza wamiliki
kwa kuanzisha viwanda hivyo katika Mkoa wa Singida kwani vimesaidia wananchi
kupata ajira na kuweza kupata kipato kinachowasaidia kuweza kujikimu katika
maisha yao sambamba na kuongeza chachu ya pato la Taifa kwa kulipa kodi.
Katika hatua nyingine
amewaagiza wataalamu wa kilimo Mkoani Singida wakisimamiwa na wakuu wa Wilaya kufanya
utafiti wa mbegu bora za alizeti na mazao mengine ili kuongeza uzalishaji wenye
tija kwa wakulima.
Kwa upande wake Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Wilaya ya Manyoni alisema kuwa
maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo
ili kuongeza ufanisi katika uwajibikaji na ukuzaji wa uchumi katika Mkoa na
Taifa kwa ujumla.
Mhe Mtaturu alisema
kuwa pamoja na serikali kuelekeza mazao ya kipaumbele nchini ambayo ni Pamba,
Korosho, Chai, Tumbaku na Kahawa lakini pia utasisitizwa uzalishaji wa zao la
Alizeti ambalo limekuwa zao tija kwa wakulima na zao kubwa la biashara katika
Mkoa wa Singida.
0 comments:
Post a Comment