Wednesday, 28 July 2021

RAIS SAMIA APATA CHANJO YA CORONA

 


“Leo tunazindua uchanjaji Tanzania tukijua chanjo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya Watu, kama alivyosema Waziri wapo wanaozikataa lakini wanaozitaka ni wengi sana, nina meseji nyingi Watu wakiuliza Mama chanjo lini chanjo lini?” amesema Rais Samia Suluhu mapema leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua uchanjaji chanjo ya corona Tanzania.
Rais Samia amesema,“Niwahakikishie Watanzania wale wote ambao kwa hiari yao wapo tayari kuchanjwa tutahakikisha chanjo zinapatikana, chanjo ni hiari ya Mtu lakini pia chanjo ni imani, mwilini mwangu hii chanjo ya leo ni ya sita, tulichanjwa tangu nikiwa Shule ya Msingi na zimenipa uzima wa kutosha mpaka leo nipo hapa…
“...Wakati ule tukiwa tunachanja wapo Wazee walikataza lakini Shuleni tulilazimishwa tukachanja, yapo madhara kuna waliovimba mikono mpaka leo wana makovu lakini tulichomwa,” amesema Rais Samia.


Rais Samia amesema Tanzania imeagiza dozi zaidi za chanjo ya Johnson and Johnson kupitia Umoja wa Afrika (AU) kama alivyoshauriwa na mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika (Africa CDC) DkJohn Nkengasong, wakati alipofanya mazungumzo naye siku ya jumanne .

“Kwa walio tayari kuchanjwa tutahakikisha wanaipata ..chanjo ni imani . Mimi nimechanjwa mara tano au sita… tumeagiza chanjo kupitia AU hili watanzania wapate kwa wingi,” amesema Rais Samia.

Serikali kupitia wizara ya Afya nchini humo imesema dozi za chanjo zitapelekwa katika kila mkoa wa taifa hilo ili kuhakikisha kwambawatu wanachanjwa.

Mkurugenzi wa Kinga Leonard Subi amesema wameamua kupeleka chanjo katika kila mkoa ili kutowabagua wanaotaka kuchanjwa kinyume na mpango wa hapo awali wa kuipeleka chanjo katika mikoakumi mikubwa.

Chanjo hiyo itatolewa kwa usawa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake.

-HABARI LEO

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA