Tuesday, 3 May 2022

RAIS SAMIA : NIMEELEKEZA SHERIA ZA HABARI ZINAZOLALAMIKIWA ZIREKEBISHWE

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wadau wa Vyombo vya Habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Sheria za Habari ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kubinya uhuru vya vyombo vya habari zirekebishwe.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Mei 3 ,2022 wakati akiwahutubia Wadau wa Vyombo vya Habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha.

“Nimeelekeza Sheria zirekebishwe lakini kwa majadiliano pande zote na sit u kwamba sisi tunataka nini. Nimemwelekeza Waziri (Nape Nnauye) sheria za habari zirekebishwe kwa kushirikisha wadau wote”,amesema Rais Samia.

"Tunatumia busara  lakini sheria zipo pale pale. Busara ninayotumia, ukinikuna vizuri mimi nitakukuna na kukupapasa huku nakupuliza ufuuuu lakini ukinipara nitakuparura,twende tufanye kazi kwa uungwana, twende tufanye  kazi kwa kuelewana", amesema Rais Samia.

 Waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika maendeleo, kwanini mimi nifanye kazi bila waandishi wa habari. Hivyo hatuhitaji kugombana, tukae tuzungumze tujenge nchi yetu",amesema Rais Samia.

"Kuna sheria zinawalinda lakini jilindeni wenyewe.. mlinzi mzuri wa maisha yako ni wewe mwenyewe",amesema Rais Samia.

 Rais Samia pia ameshauri waandishi wa habari kuwa Wazalendo kwa kuandika mambo mazuri za kutetea Bara la Afrika huku akiwataka waandishi wa habari kuzitangaza mila na desturi nzuri za Tanzania.

“Tunazo mila na desturi tunapaswa kuzilinda, na nyinyi waandishi wa habari mnatakiwa kuzilinda ili kuepuka mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu. Baadhi ya watu wanapost picha chafu mtandaoni, wanajianika mtandaoni, wengine wanafanya hivyo kwa kututojua madhara ya kufanya hivyo. Wa kwenda kuzionesha changamoto za kidigitali.” ,amesema Rais Samia.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA