Binti auwawa kwa 'kosa la ndoa' India
Mauji kama haya sio jambo la kawaida kutokea maeneo ya Kusini mwa India
Polisi nchini India wamesema kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 26 mtaalamu wa Kompyuta, amepatikana akiwa amenyongwa nyumbani kwao.
Wazazi wa mwanamke huyo ambao wanazuiliwa na polisi wamekiri kumuua binti yao kwa sababu aliolewa kinyume na matakwa yao.
Mwanamke huyo aliolewa na mfanyakazi ,mwenzake kutoka jamii tofauti siku chache zilizopita.
Maafisa wanasema kuwa mauaji kama haya sio kawaida kutokea maeneo ya Kusini mwa India.
NA BBC
0 comments:
Post a Comment