Monday 17 March 2014

Jeshi la DRC lakomboa mji wa Lukweti


Wanajeshi wa DRC wakiwa kwenye gari la kijeshi katika harakatai zao kupambana na wapiganaji
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo limesema kuwa limekomboa mji mmoja Mashariki mwa nchi ambao jamii moja ilikuwa inautumia kama makao yake makuu kwa miaka sita.
Mji huo unajulikana kama Lukweti - na uko takriban kilomita themanini kaskazini mwa mji wa Goma.
Kundi hilo nalo linajulikana kama APCLS (Alliance for a Free and Sovereign Congo).
Mji huo uko katika jimbo la Masisi , katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambako jeshi la Congo likisaidiwa na kikosi maalum cha UN limekuwa likiwasaka waasi.
Kundi hilo lilizinduliwa mwaka 2008 na watu wa jamii ya Hunde ambao wamekuwa wakipambana vikali na watu wa jamii ya Tutsis katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
ktk bbc

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA