Monday 17 March 2014

Malaysia:Kauli ya mwisho ya rubani mwenza



Picha ya ukaguzi uliofanywa na rubani kabla ya ndege kuruka
Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA