Monday, 28 April 2014

ANGALIA PICHA YA POLISI WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUIBA MTOTO


Mwanamama ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).

SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 na picha yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili isionekane, hatimaye Ijumaa Wikienda limeinasa.


 Askari huyo ambaye kituo chake ni Ilala jijini Dar, alikamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7) aliyeibwa April 6, mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

 Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana na baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile umri miaka 20) kuwa Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona mtoto aliyezaliwa ndipo akatoroka naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi.

 Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 17, mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa Makao Makuu ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
 Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku hiyo mama huyo alikuwa katika harakati za kutokomea kusikojulikana lakini bahati nzuri polisi waliimarisha ulinzi.
 “Alikuwa ndiyo yupo katika mikakati ya kutoroka na haikujulikana alikuwa anataka kwenda wapi maana tayari alishajua kuwa anatafutwa hivyo kutapatapa na kuingia kirahisi katika mkono wa sheria,” kilisema chanzo hicho.
 Baada ya kuhojiwa na polisi kujiridhisha na tuhuma hizo za wizi, mstakiwa huyo alipandishwa katika mahakama ya…na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
 Baada ya kusomewa mashtaka siku hiyo, kesi iliahirishwa hadi Mei 6, mwaka huu ambapo mshtakiwa aliruhusiwa kupata dhamana lakini akashindwa kutimiza masharti (wadhamini wawili na hati) hivyo kurudishwa sero hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
 Kwa mujibu wa chanzo chetu, kabla ya kunaswa katika tukio hilo, askari huyo anayedaiwa kuwa ni mama wa watoto, aliolewa na kuachika miaka kadhaa iliyopita.
NA GPL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA