Wednesday 16 April 2014

COPA del REY-EL CLASICO LEO, REAL KUMKOSA RONALDO, ANCELOTTI AJIAMINI!

BILA mchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, Real Madrid wanaingia kata EL CLASICO ya 3 na ya mwisho kwa Msimu huu dhidi ya FC Barcelona usiku wa leo katika uwanja wa Estadio Mestalla Mjini Valencia.
Hii ni fainali ya Fainali ya Kombe la Mfalme, Campeonato de España – Copa de Su Majestad el Rey, kwa kwetu limezoeleka kwa jina la  Copa del Rey.
Barcelona, ambao wameshatwaa Kombe hili mara 26, mara ya mwisho kulitwaa ni 2012, wakati Real, ambao wamelitwaa mara 18, Mwaka Jana walifungwa katika mechi ya fainali na mahasimu wao Atletico Madrid.
Barca na Real zimeshakutana mara mbili Msimu huu kwenye mechi za ligi kuu maarufu kama La Liga, huku  Barca wakishinda Mechi zote mbili.
 Mara ya mwisho kukutana kwenye Copa del Rey ni Mwaka 2011, tena Uwanja huu huu wa safari hii, Estadio Mestalla, ambapo Bao la Dakika za Majeruhi la Cristiano Ronaldo liliwapa Kombe Real na pia kumpa Kombe la Kwanza Kocha Jose Mourinho kwenye himaya yake na Real Madrid.
MECHI 3 ZILIZOPITA:
-Real 3 (Benzema 2, Ronaldo) Barcelona 4 (Iniesta, Messi 3), La Liga, Machi 2014
-Barcelona 2 (Neymar, Sanchez) Real 1 (Jese), La Liga, Oktoba 2013
-Real 2 (Benzema, Ramos) Barcelona 1 (Messi), La Liga, Machi 2013
Lakini safari hii kila Klabu ina Meneja mpya, Carlo Ancelotti na Real na Gerardo Martino kwa Barca, na wanatinga kwenye Fainali hii wakitokea kwenye matokeo tofauti kabisa.
Barca wanatinga Fainali hii wakiwa kwenye majonzi makubwa kwani Wiki moja iliyopita walikuwa kwenye ndoto kubwa ya kutwaa Trebo kama walivyofanya Mwaka 2009 lakini mambo yakapinduka na wakatolewa toka UEFA na Atletico Madrid na Siku 3 baadae kufungwa 1-0 na Granada kwenye La Liga na kuachwa wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Atletico na Real huku Mechi zikiwa zimebaki 5.
Tofauti kabisa, Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na morali ya juu baada ya kufuzu kuingia Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia kuwa kileleni mwa La Liga, pamoja na Atletico, baada ya kuifumua Almeria 4-0 Siku 3 baadae.
Kila Timu inakabiliwa na Majeruhi wengi huku Barca ikiwa dhoofu kwenye safu yao ya ulinzi wakiwemo Gerard Pique, Carles Puyol na Marc Bartra, ambaye kidogo ni nafuu na huenda akacheza, lakini upo uwezekano mkubwa kwenye Mechi hii Difensi ya Barca ikawa na Viungo, Mascherano na Busquet, kama Masentahafu wao.
Real wataingia wakiwa na hatihati kuhusu kucheza kwa Staa wao Cristiano Ronaldo ambae hajacheza Mechi 2 zilizopita akiwa na maumivu.
Carlo Ancelotti ameleeleza jana kuwa Ronaldo hatakuwepo, lakini kukosekana kwake kunaweza kutoa mwanya kwa ama Asier Illarramendi au Isco kucheza na kuungana na Angel di Maria, Gareth Bale na Karim Benzema kwenye mashambulizi.
Ancelotti mapema jana alikaririwa akisema Ronaldo anaweza kucheza kwasababu anaendelea vizuri, lakini baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya leo alithibitisha kuwa nyota huyo atakosekana kabisa.
“Cristiano Rinaldo hatakuwepo, lakini tuna wachezaji wengi katika kikosi chetu”.
“Tuna imani kubwa na timu hii. Nimekuwa nikijitahidi kukabiliana na majeruhi na nadhani tutafanya kazi nzuri tu”. Aliongeza kocha huyo raia wa Italia ambaye hata hivyo aligoma kutaja kikosi kinachoweza kuanza leo hii.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao; Modric, Alonso, Illarra; Di Maria, Benzema, Bale
Barcelona: Pinto; Alves, Mascherano, Bartra, Alba; Busquets, Xavi, Iniesta; Neymar, Messi, Sanchez
COPA del REY-NJIA YA FAINALI
NUSU FAINALI
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2]
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0          Real Madrid CF 2 [0-5]
Jumatano Februari 12
Real Sociedad 1 FC Barcelona 1 [1-3]
FAINALI
Aprili 16
Real Madrid v Barcelona

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA