Wednesday, 30 April 2014

KENYA::RUKSA KUOA WAKE WENGI




Baadhi ya wanawake wanapinga sheria inayoruhusu wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja
Sheria inayoruhusu wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja, imepitishwa nchini Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria hio licha ya malalamiko kutoka kwa vikundi vya wanawake nchini humo.
Taarifa kutoka katika ofisi ya Rais ilisema kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengee kadhaa kuhusu ndoa , imekuwa sheria sasa.
Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.
Taarifa ya Rais ilisema kuwa "ndoa ni muungano wa watu wawili mwanamke na mwanamume , ikiwa mume atataka kuoa mke mmoja au wawili, mwenyewe anapaswa kuamua. ''
Mswaa wa awali, ulimpa mwanamke haki ya kwenda mahakamani kupinga mume wake kuoa mke wa pili, lakini wabunge wanaume waliungana katika kuunga mkono mswada huo.

Wabunge wanaume waliungana licha ya vyama vyao kupitisha mswada huo
Wakati mswada huo ulipopitishwa mwezi jana , wabunge wanawake waliondoka bungeni kwa Hasira baada ya mjadala mkal
Viongozi wa baadhi ya makanisa pia wamepinga vikali mswada huo
Shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani.
Katika sehemu nyingi barani Afrika, kuoa zaidi ya mwanamke mmoja ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi sawa na hali ilivyo nchini Kenya na hata pia miongoni mwa waumini wa dini ya kiisilamu.
Wengi wanasema kuwa sheria hiyo inapiga tu muhuri wa utamaduni uliopo.
na BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA