Wednesday 9 March 2022

PROF. MBARAWA ATOA SIKU 14 UJENZI DARAJA LA TAZARA


Muonekano wa reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji mkoani Morogoro.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akifanya mawasiliano na wataalam mbalimbali katika kutafuta ufumbuzi wa haraka wa ukarabati wa reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji hivi karibuni mkoani Morogoro.



Eng. James Mwasha wa TAZARA akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji mkoani Morogoro.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Eng. Allan Singo (kulia) na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Eng. Alinanuswe Lazeck (kushoto),  walipokagua miundombinu ya barabara na reli mkoani humo. 



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na viongozi wa TAZARA alipokagua ukarabati wa reli hiyo sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 ambayo imesombwa na maji hivi karibuni mkoani Morogoro.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametoa siku 14 kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA kukamilisha ujenzi wa daraja lililosombwa na maji  katika sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 mkoani Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kukagua eneo hilo Prof. Mbarawa amewataka watendaji hao kushirikiana na watendaji wenzao wa TANROADS na TRC ili eneo hilo likamilike haraka na safari za treni za mizigo na abiria ziendelee.

“Hakikisheni katika muda wa siku 7 hadi 14 sehemu hii inakamilika, ujenzi ufanyike mchana na usiku ili kuirudisha reli katika hali yake ya kawaida na hivyo kuondoa usumbufu kwa wateja wenu”, amesisistiza Prof. Mbarawa.

Reli ya TAZARA sehemu ya Fuga-Kisaki KM 211 mkoani Morogoro ilisombwa na maji Februari 14 mwaka huu na kuathiri huduma za usafiri na uchukuzi wa reli hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa TAZARA Eng. Bruno Ching’andu amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa jitihada za kuwawezesha kupata vifaa vya kujenga daraja hilo na kumhakikishia litakamilika na huduma kurejea katika kipindi cha wiki mbili.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA