Thursday, 3 April 2014

Malaysia haitakata tamaa kutafuta ndege


Waziri mkuu wa Malaysia Najib Raza azuru Australia
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak amewasili jijini Perth, magharibi mwa Australia, ambako shughuli ya kutafuta ndege ya MH370 inaendelea ili kuwashukuru wale wote wanaohusika na shughuli ya kusaka mabaki ya ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka majuma matatu yaliyopita .

Bwana Najib atakutana na waziri mkuu wa Australia Tony Abbott na Angus Houstun ambaye ni mkuu wa jeshi aliyestaafu na wote wanaosimamia shughuli hiyo.
Kadhalika bwana Najib amesema kuwa Malaysia haitaka tamaa kuitafuta ndege hiyo.
Ndege hiyo ya Malayisa ilipotea tarehe nane mwezi machi wakati ilipokuwa ikifanya safari ya kwenda Kuala Lumpur kutoka mji wa Beijing. Ilikuwa imewabeba abiria 239.
Ndege na meli kadhaa zimekuwa zikizunguka eneo la kusini mwa bahari Hindi, ambako ndege hiyo inaaminika kuwa ilianguka.
Tayari meli moja ya Uingereza imewasili huko kuchangia juhudi hizo.
Jamaa wa ndege ya Malaysia MH370 waandamana
Mahala panapoendeshewa shughuli ya kuitafuta imepanuka hadi kilomita laki mbili magharibi mwa mji wa Perth nchini Australia.
Lakini kufikia sasa hakuna lolote lililoonekana kuasharia uwezekano wa ndege hiyo kupatikana pahala hapo.
Waziri mkuu Najib Razak wa Malaysia amekutana na kikosi kinachoendesha shughuli hiyo asubuhi hii kabla ya kuendeleza kazi hiyo.
Pia waziri huyo atatembelea shirika linaloongoza shughuli ya kutafuta ndege hiyo.
Familia na jamaa ya abiria 153 kutoka China wameshtumu vikali serikali ya Malaysia kwa kutowapa habari zozote kuhusiana na jamaa wao ambao walikuwa miongoni mwa abiria 239 waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Beijing Uchina
NA BBC

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA