Saturday 21 May 2016

TIKETI ZA BAHATI NASIBU YA TAIFA ZAANZA KUUZWA ,MSHINDI WA KITITA CHA MILIONI 100 KUJULIKANA JUMAMOSI


Mwenyekiti wa kampuni ya  Gidani  ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Profesa Bongani Aug Khumalo,akitoa maelekezo ya mchezo huo kwa waandfishi wa habari na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi, (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba  na katikati ni Meneja mradi wa  Kampuni hiyo,Brett Smith

Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya  Michezo ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akijaribu mashine za michezo zinavyofanya kazi

Kampuni ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo  ambayo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kushiriki  bahati nasibu inayoendeshwa kitaalamu na inayowezesha  washindi kujishindia donge nono  na kubadilisha maisha yao.


Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akitoa maelekezo kwa  Maofisa waandamizi wa kampuni ya Gidani


“Zawadi ya milioni 100 sio  ndogo  itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi na kushiriki katika mchezo huu.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.


Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya  uzinduzi wa kuuza tiketi
“Tiketi za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi wengi kushinda”Alisema.

Alisema mbali  na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 1,000.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya  uzinduzi wa kuuza tiketi




Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya  uzinduzi wa kuuza tiketi


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA