26 wauawa katika shambulizi Borno,Nigeria
Mashambulizi yaliyofanywa awali na Boko Haram katika mji wa Jos
Kundi la
wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wametuhumiwa kwa kuwaua watu 26
katika mashambulizi dhidi ya kijiji kimoja Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria , karibu na eneo ambalo wasichana zaidi ya miambili walitekwa
nyara.
Watu waliokuwa wamejihami waliwaua watu tisa katika kijiji cha Shawa na wengine kumi na saba katika kijiji cha Alagarno.
Hili ni
shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria wakati nchi hiyo
ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana miambili
waliotekwa nyara na Boko Haram.Eneo hilo liko karibu na mji wa Chibok
ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara mwezi jana na kundi
la Boko Haram.
Juhudi hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel, Marekani na Uingereza.
Pia
limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika
jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi
wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos,
lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali
kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.
Wanakijiji
wanasema kuwa wapiganaji hao walisawili katika kijiji hicho usiku wa
manane na kuwalazimisha watu kutoroka na kujificha vichakani.
Inaarifiwa waliondoka baada ya saa nne za usiku wakiwa wamebeba chakula walichoiba pamoja na magari.
0 comments:
Post a Comment